GACHAGUA ATETEA MSIMAMO WA HISA, AKISEMA ODM WAMEIGA
Aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua, ametetea msimamo wake wa kupigania hisa za eneo la Mlima Kenya serikalini, akisema msimamo sawa umechukuliwa na chama cha ODM kinapopanga ushirikiano wa kisiasa na UDA.
Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga nchini, Gachagua ambaye pia ni kinara wa chama cha DCP, amesisitiza kwamba kila upande kwenye ushirikiano huo unataka kufahamu asilimia ya nyadhifa za serikali itakayopewa kila chama kabla ya ushirikiano.
Ametaja ukosoaji dhidi yake kama unafiki.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































