KENYA YAJIUNGA NA MPANGO WA KIMATAIFA WA AFYA
Katika juhudi za kupunguza vifo vya watoto wachanga, Kenya imetangaza kujiunga na mpango wa kimataifa wa afya kwa muda wa miaka 5, mpango utakaogharimu kima cha shilingi bilioni 11.
Kulingana na mkurugenzi mkuu wa idara ya afya Daktari Patrick Amoth, mpango huo utatekelezwa katika kaunti 12 ambazo huchangia asilimia 50 ya vifo hivyo, akisema kaunti ya Nakuru itakuwa ya kwanza kunufaika.
Miongoni mwa kaunti nyingine ni Trans Nzoia, Kakamega, Kisumu, Nairobi, Mombasa na Uasin Gishu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































