#Local News

UPASUAJI WA MAITI KUENDELEA KERICHO

Imebainika kwamba watoto 4 kati ya 25 waliofukuliwa kutoka kaburi la pamoja kwenye kaunti ya Kericho walifariki kutokana na majeraha ya kichwa, huku wengine 10 wakifariki baada ya kuzaliwa kabla ya siku zao kufika.

Kulingana na ripoti ya upasuaji wa maiti iliyoongozwa na mwanapatholojia wa serikali Dakta Richard Njoroge, miili ya waathiriwa ilikuwa katika hatua mbali mbali za kuharibika, michache tu ikionekana kufariki siku chache zilizopita.

Miili ya watu wazima imeratibiwa kufanyiwa upasuaji hii leo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *