#Football #Sports

LEOPARDS MGONGONI PA GOR KUFUATIA USHINDI

Klabu ya AFC Leopards iliweka wazi nia yake ya kuwania ubingwa wa taji la ligi kuu ya soka nchini, KPL, kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kariobangi Sharks ugani Nyayo hapo jana.

Kwa sasa wanawaandamana viongozi wa ligi hiyo Gor Mahia, kwa pointi 4 pekee ingawa Gor wana mechi moja mkononi.

Bao la pekee lake Tyson Otieno kunako dakika ya 59 lilitosha kuwapa Ingwe pointi 3 muhimu, ligi hiyo inapoingia kwenye mkondo wa lala salama.

Ingwe wa pointi 52 baada ya mechi 26, Gor Mahia wakisalia kileleni na pointi 56.

Kwingineko, Shabana FC waliizima Murang’a Seal kwa kichapo sawa ugani Gusii, kufuatia bao la pekee la Wycliffe Omondi katika dakika ya 40.

Shabana wana pointi 43, wakiwa na uwezo wa kutwaa taji hilo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

LEOPARDS MGONGONI PA GOR KUFUATIA USHINDI

WAKENYA WAWIKA BERLIN

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *