UPINZANI: RUTO ANATAKA KUWATUMIA WAFU KUSHINDA
Viongozi wa muungano wa upinzani wameratibiwa kuendelea na ziara yao katika eneo la Ukambani hii leo, baada ya kuanza ziara hiyo hapo jana katika kaunti ya Makueni.
Kwenye ziara hiyo, viongozi hao wameibua madai kwamba Rais William Ruto ana nia ya kujilazimishia ushindi kwenye uchaguzi mkuu ujao kwa kutumia kura za wakenya waliofariki ila maelezo yao yangali kwenye sajili ya tume huru ya uchaguzi na mipaka, IEBC.
Wameshinikiza sajili ya wapiga kura kusafishwa ipasavyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































