#Football #Sports

SILVA ATANGAZA KUONDOKA MAN CITY

Nahodha wa klabu ya Manchester City Bernardo Silva, amearipotiwa kuiarifu klabu hiyo kuhusu kuondoka kwake mwishoni kwa msimu huu.

Kandarasi ya kiungo huyo raia wa Ureno mwenye umri wa miaka 31, itakamilika mwezi Juni mwaka huu, na ameonyesha ari ya kujiunga na klabu kadhaa bila ada yoyote.

Silva alijiunga na City mwaka wa 2017, na kumfanya awe mechezaji wa tatu kuwahi kuhudumu katika klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi baada ya John Stones na Phil Foden.

Akiwa amepumzishwa na timu ya taifa ya Ureno kwenye mechi za kirafiki zinazoendelea, nyota huyo wa zamani wa Monaco ametumia likizo yake kutafakari kuhusu mustakabali wake.

Vyombo vya habari kadhaa barani Ulaya vimeripoti kwamba Silva amewaambia wasimamizi wa City kwamba hataki kupewa mkataba mpya.

Kipaumbele chake ni kusalia bara Ulaya, ripoti zikiarifu kwamba Barcelona na Juventus zinawania sahihi yake.

Klabu nyingine ni Galatasaray ya Uturiki, klabu za Marekani na Saudi Arabia.

Nyota huyo amekuwa na kipindi cha kuridhisha nchini Uingereza, akishinda mataji 6 ya EPL, na huenda akafikisha 7 mwezi Mei, iwapo City wataipiku Arsenal kwenye kampeni hiyo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *