#Local News

KINDIKI AWATAKA MABALOZI KUITANGAZA KENYA

Naibu Rais, Kithure Kindiki, amewataka mabalozi wa Kenya kuitangaza nchi kama salama na yenye fursa za uwekezaji, akisema ni jukumu lao kuvutia wawekezaji na wageni.

Akizungumza wakati wa kufunga kongamano la 19 la mabalozi jijini Nairobi, Kindiki amesisitiza umuhimu wa mabalozi kushiriki kikamilifu katika kukuza taswira ya taifa kimataifa.

Aidha ameongeza kuwa Kenya imepiga hatua kubwa kiuchumi, na kuhimiza juhudi zaidi za kutangaza mafanikio hayo ili kuchochea uwekezaji na maendeleo ya nchi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

KINDIKI AWATAKA MABALOZI KUITANGAZA KENYA

SILVA ATANGAZA KUONDOKA MAN CITY

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *