NAIBOIS, MARA SUGAR KUVAANA KPL
Ligi kuu ya soka ncini KPL inarajelewa hii leo ambako Nairobi United watamenyana na Mara Sugar katika uwanja wa Ulinzi Sports Complex, katika vita vya katikati mwa jedwali la ligi.
Naibois walio katika nafasi ya 10 wakiwa na pointi 34 baada ya mechi 24, wamekuwa na msimu vuguvugu, wakiandikisha matokeo mseto.
Mechi yao ya mwisho iliishia katika sare tasa dhidi ya APS Bomet.
Kwa upande wao, Mara Sugar wataingia uwanjani wakiwa katika nafasi ya 12 kwa pointi 30 baada ya mechi 25, wakiwa bado wanapambana kusalia kwenye ligi kuu wanayoshiriki kwa msimu wa pili katika historia yao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































