WETANG’ULA ATISHIWA KESI MAHAKAMANI
Kundi la Linda Mwananchi limetishia kumshtaki Spika wa Bunge la Kitaifa, Moses Wetang’ula, kwa kumfurusha Mbunge wa Kitutu Chache Kusini, Anthony Kibagendi, kutoka vikao vya bunge.
Viongozi hao wamedai kuwa hatua hiyo ilikiuka uamuzi wa mahakama uliotaka mbunge huyo arejeshwe bungeni baada ya kuondolewa awali.
Kibagendi alitimuliwa kutokana na matamshi yake kuhusu ufisadi bungeni, suala ambalo sasa limeibua mvutano mpya wa kisheria na kisiasa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































