ODUOR ALENGA NAFASI YA KUDUMU STARS
Kiungo wa ulinzi wa Harambee Stars, Clarke Oduor, analenga kujihakikishia nafasi ya kudumu katika kikosi hicho baada ya kuchangia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Grenada kwenye mashindano ya kimataifa jijini Kigali.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, anayekipiga kwa mkopo katika klabu ya Grimsby Town kutoka Bradford City, ameonyesha kiwango kizuri katika kurejea kwake kikosini baada ya karibu miaka sita.
Akiwa amelelewa katika akademia za Leeds United na Barnsley, Oduor ameonyesha ubora wake kwa kucheza nafasi mbalimbali za kiungo na ulinzi kwa utulivu na uelewa wa mchezo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































