TUCHEL: FODEN HANA UHAKIKA NA NAFASI YA KOMBE LA DUNIA
Kocha wa uingereza, Thomas Tuchel, amesema nafasi ya Phil Foden katika kikosi cha Kombe la Dunia haijahakikishwa, baada ya mchezaji huyo kushindwa kuonyesha kiwango cha juu tena katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Japan.
Foden, mwenye umri wa miaka 25, alikumbana na changamoto kucheza katika nafasi isiyo ya kawaida mbele, huku Harry Kane akikosa kwenye mchezo huo.
Hali hii imeongeza mashaka kuhusu nafasi yake, huku pia akishuka katika mpangilio wa wachezaji chini ya Pep Guardiola katika klabu ya Manchester City katika wiki za hivi karibuni.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































