#Rugby #Sports

BUNGOMA HIGH YALENGA UBINGWA WA RAGA

Timu ya raga ya Bungoma High School inalenga kurejea historia ya mwaka 2016 kwa kutwaa ubingwa wa kitaifa wa raga ya wachezaji 15 katika michezo ya shule za upili itakayofanyika Kisumu

Hii ni baada ya ushindi wao wa kanda ya magharibi walipowashinda Kakamega School alama 12-07 katika fainali iliyofanyika Chavakali High School mwezi uliopita.

Kocha wao, Titus Wangila, ana imani kikosi chake kina uwezo wa kuwashinda wapinzani wakubwa na kutwaa taji hilo, hasa baada ya mabingwa watetezi Vihiga High School kuondolewa mapema.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *