#Local News

MOTO WATEKETEZA NYUMBA ZA MAGEREZA LANG’ATA

Idara ya magereza nchini imethibitisha kuwa moto umeteketeza nyumba 30 za makazi ya maafisa katika Gereza la Wanawake la Lang’ata lenye ulinzi mkali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na idara hiyo moto huo ulizuka Jumatano jioni majira ya saa moja na nusu na kuteketeza nyumba hizo kabisa.

Hata hivyo, idara hiyo imesema hakuna mtu aliyepoteza maisha au kujeruhiwa, huku kikosi cha dharura kikifanikiwa kudhibiti moto huo na kuzuia usienee zaidi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *