#Local News

VITUO 30 VYA AFYA KUSHTAKIWA KWA ULAGHAI WA SHA

Wamiliki na wakurugenzi wa vituo 30 vya afya wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za ulaghai iwapo Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma atatoa idhini ya mashtaka hayo.

Kurugenzi ya Upelelezi wa Jinai imesema uchunguzi wa malalamishi ya ulaghai pamoja na ukaguzi wa kitaalamu wa miamala ya vituo hivyo umebaini kuwa wote wana kesi ya kujibu.

Tayari vituo 18 vya afya pamoja na watu 50 wamefikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashtaka ya ulaghai.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *