#Local News

UHABA WA MAFUTA WAKUMBA KAKAMEGA

Madereva katika mji wa Kakamega wanakabiliwa na uhaba wa mafuta uliosababisha usumbufu mkubwa katika usafiri na shughuli za kila siku.

Kwa mujibu wa baadhi ya madereva, vituo vingi vya mafuta mjini humo vimeishiwa na mafuta, huku ni vituo viwili pekee vinavyoripotiwa kuwa bado vina akiba, hali ambayo imelazimisha madereva kusafiri umbali mrefu kutafuta mafuta, huku baadhi ya vituo vilivyosalia vikifungua kwa muda mfupi, hasa nyakati za jioni.

Madereva pia wanadai kuwa katika maeneo kadhaa ya kaunti hiyo, bei ya mafuta imepanda hadi shilingi 200 kwa lita, ingawa mjini Kakamega bei bado iko karibu shilingi 178 kwa lita licha ya upatikanaji kuwa wa kusuasua.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *