#Local News

WALINZI WAWILI WAUAWA SANG’ALO – BUNGOMA

Hali ya taharuki imetanda katika eneo la Sang’alo, kaunti ya Bungoma, baada ya walinzi wawili kuvamiwa na watu wanaoshukiwa kuwa wahalifu.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa Bungoma Kaskazini, William Letting, mmoja wa walinzi hao alipoteza maisha papo hapo huku mwenzake akiaga dunia alipokuwa akipokea matibabu hospitalini.

Wakaazi wa eneo hilo wamelalamikia kuongezeka kwa visa vya uhalifu na ukosefu wa usalama, huku kamanda huyo akiamuru maafisa wa polisi katika eneo hilo kuhamishwa ili kuboresha hali ya ulinzi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *