#Local News

MZOZO MWINGI: WASAFIRI WAKWAMA 

Shughuli za uchukuzi zimeendelea kutatizika kwenye barabara kuu ya Mwingi kuelekea Garissa kutokana na hali tete ya usalama iliyochochewa na kuuawa kwa watu wanane mwishoni mwa wiki jana kwenye uvamizi.

Mzozo huo unaohusisha jamii mbili kutoka kaunti jirani, umesababisha kufungwa kwa barabara hiyo huku wasafiri wakikwama katika vituo vya mabasi ya usafiri.

Tayari muungano wa KUPPET umeitaka serikali kuhakikisha usalama wa walimu eneo la kaskazini mashariki.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *