#Rugby #Sports

KCB YAJIIMARISHA KABLA YA FAINALI KENYA CUP

Klabu ya raga ya KCB RFC imeimarisha maandalizi yake kwa fainali ya dimba la Kenya Cup dhidi ya Kabras RFC litakalochezwa tarehe 9 mwezi ujao mjini Kakamega.

Kocha mkuu wa klabu hiyo Andrew Amonde amesema kuwa wanabenki hao wanalenga kurekebisha makosa yaliyosababisha kupoteza kwao katika fainali zilizopita dhidi ya Kabras mwaka wa 2023 na 2024.

Amesema kuwa wanaangazia pakubwa kujiandaa kisaikolojia kwa pambano alilolitaja kuwa kubwa na kwamba hawatakata tamaa.

Wanabenki hao walikata tiketi ya fainali baada ya kuwalaza Nondescript 52-7 katika semi fainali huku Kabras wakiwakaragaza Blak Blad 48-15 kwenye semi fainali nyingine.

KCB RFC watajivunia kurejea kikosini kwa wachezaji wanne wanaochezea timu ya taifa ya Shujaa.

Wanne hao ni Samuel Asati, Festus Shiasi, Floyd Wabwire na George Ooro.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KCB YAJIIMARISHA KABLA YA FAINALI KENYA CUP

MZOZO MWINGI: WASAFIRI WAKWAMA 

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *