#Local News

RUTO AKOSOA WANAOPINGA MIRADI

Rais William Ruto amewakosoa baadhi ya viongozi wanaopinga maendeleo ya miundombinu, akisema kauli zao hazina msingi na zinapotosha umma.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Leba kaunti ya Vihiga, Rais amesema kuna wanaodai kuwa barabara zinazojengwa hazina maana, licha ya manufaa yake kwa wananchi, na kushangaa kwa nini hawakutoa maoni wakati miradi ya barabara na reli ilipokuwa ikianzishwa.

Aidha, ameeleza kutoridhishwa na ukosoaji huo, akisisitiza kuwa serikali itaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo kwa manufaa ya taifa bila kuyumbishwa na upinzani huo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *