#Local News

MUDAVADI AUNGA MKONO RUTO 2027, ASISITIZA AWAMU MBILI

Mkuu wa Mawaziri  Musalia Mudavadi amesema kuwa tayari alionyesha mwelekeo wa kisiasa katika uchaguzi uliopita na kuwa msimamo huo bado haujabadilika kuelekea uchaguzi wa 2027.

Mudavadi amesisitiza kuwa njia ni ile ile, akieleza wazi kuwa anamuunga mkono Rais William Ruto kuendelea kuongoza kwa muhula mwingine.

Ameongeza kuwa ana imani kuwa Ruto atahudumu kwa mihula miwili, akiwataka wafuasi kuungana na kuhakikisha azma hiyo inafanikishwa kupitia mshikamano wa kisiasa na uungwaji mkono wa wananchi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *