SERIKALI YATOA TAARIFA YA UCHUMI NA MAFURIKO
Msemaji wa Serikali Isaac Mwaura ametoa tathmini chanya kuhusu hali ya uchumi, huku akionya kuhusu hatari inayoongezeka ya mafuriko katika baadhi ya maeneo ya nchi.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Mwaura amesema kuwa Kenya ilizalisha ajira mpya 822,100 mwaka 2025, na kuongeza jumla ya walioajiriwa kutoka milioni 20.8 mwaka 2024 hadi milioni 21.6.
Amebainisha kuwa sehemu kubwa ya ajira hizo zilitokana na sekta isiyo rasmi, huku akisisitiza umuhimu wa kuchukua tahadhari dhidi ya athari za mafuriko yanayoweza kujitokeza.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































