#Local News

RUTO AONGEZA KIMA CHA CHINI CHA MISHAHARA KWA WAFANYAKAZI

Rais William Ruto ametangaza ongezeko la asilimia 12 ya kima cha chini cha mishahara kwa wafanyakazi nchini pamoja na nyongeza ya asilimia 15 kwa wafanyakazi wa sekta ya kilimo.

Ruto ametoa tangazo hilo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi yaliyofanyika katika kaunti ya Vihiga, akisema hatua hiyo inalenga kuboresha maisha ya wafanyakazi na kukabiliana na changamoto za kiuchumi.

Ameeleza kuwa serikali imechukua hatua hiyo kufuatia ombi la wafanyakazi kupitia COTU, akisisitiza dhamira ya serikali katika kulinda maslahi ya wafanyakazi na kuimarisha ustawi wao nchini.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *