#Football #Sports

FLICK KUSAINI MKATABA MPYA BARCELONA

Kocha wa klabu ya FC Barcelona Hansi Flick anatarajiwa kusaini mkataba mpya na klabu hiyo, baada ya mpango huo kuthibitishwa kufuatia kuchaguliwa tena kwa Rais Joan Laporta.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, mkataba mpya utadumu kwa miaka miwili ijayo, huku kukiwa na uwezekano wa kuongezwa hadi mwaka 2029 kupitia kipengele cha nyongeza.

Inaarifiwa kuwa wakala wake Pini Zahavi anatarajiwa kuwasili hivi karibuni kukamilisha maelezo ya makubaliano hayo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *