NI WAKATI WA VIWANDA KUNAWIRI: DIDMUS
Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa, ametetea mapendekezo ya mswada wa kifedha wa mwaka 2024-25, akisema mapendekezo haya yatalinda watengenezaji wa bidhaa humu nchini na hivyo kubuni nafasi za ajira.
Akizungumza bungeni wakati wa kikao kinachoendelea, Barasa amewalaumu wabunge wa upinzani kutokana na kudorora kwa hali ya uchumi hapa nchini.
Kulingana na mbunge huyo, mswada huo utawezesha ujenzi wa viwanda humu nchini.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































