NAIROBI KUWA MWENYEJI WA MAONYESHO YA 8 YA AGRO-FOOD PACK
Toleo la 8 la Maonyesho ya Agro-Food linatazamiwa kufanyika eneo la Sarit centre jijini Nairobi kuanzia tarehe 8 hadi 10 Agosti.
Toleo hilo la kila mwaka linalosifika kwa michango yake kwa tasnia ya chakula na kampuni mbali mbali za uzalishaji na huandaliwa na kampuni ya hafla ya MXM Exhibitors yenye makao yake Dubai.
Akizungumza kuhusu maonyesho hayo Axan Rashid ambaye ni mkurugenzi mkuu wa maandalizi hayo amesema kuwa Maonyesho hayo yataleta Pamoja makundi muhimu na wadau katika sekta ya kilimo na chakula, na vile vile yatatoa jukwaa la mitandao, uvumbuzi, na kuonyesha maendeleo ya hivi karibuni katika teknolojia na bidhaa.
Aidha ametaja kuwa toleo la nane linalenga jukwaa la kuhamisha teknolojia, kukuza biashara kati ya Kenya na nchi nyingine 40 kutoka bara Ulaya na bara Asia.
Imetayarishwa na Maureen Amwayi
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































