#Football #Sports

GOR MAHIA WAKASHIFU UHUNI

Meneja wa Timu ya Gor Mahia Victor Nyaoro amekashifu uhuni unaoshuhudiwa siku za hivi majuzi unaofanywa na baadhi ya mashabiki wanaodai matokeo mema kutoka kwa mabingwa hao wa rekodi.

Kulingana na Nyaoro, inasikitisha kwa kocha ambaye amekuwa na timu hiyo kwa muda wa miezi sita hivi na benchi la ufundi kuzongwa na mashabiki wa klabu hiyo, akisema uhuni hauwezi kutatua hali iliyopo klabuni.

Nyaoro anasema ni mapema mno kutoa uamuzi kwa timu, akitoa wito kwa mashabiki kutafuta njia mbadala za kueleza malalamishi yao.

Jumapili iliyopita, kocha mkuu Leonardo Martins Neiva alishambuliwa na mashabiki waliokuwa na hasira mjini Machakos baada ya Gor kushiriki kiporo na Murangá Seal.

Kabla ya hapo, nahodha wa timu hiyo Philemon Otieno alizomewa na kutukanwa, na kumlazimu kuomba msamaha baada ya Gor kufungwa 2-1 na Nairobi City Stars.

Imetayarishwa na Nelson Andati

GOR MAHIA WAKASHIFU UHUNI

BANDARI WAKO TAYARI KUMENYANA NA GOR

GOR MAHIA WAKASHIFU UHUNI

NEYMAR KUKOSA MAZOEZI KWA WIKI MBILI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *