MMUST YALENGA KUTETEA UBINGWA WA RAGA 7S

Chuo Kikuu cha MMUST kimejizatiti kutetea ubingwa wa raga ya wanawake ya wachezaji saba katika mashindano ya kitaifa ya Shirikisho la Michezo ya Vyuo Vikuu Kenya yatakayofanyika katika Chuo Kikuu cha Kabarak. Mwalimu wa michezo wa chuo hicho, Geoffrey Barasa, ameonyesha matumaini kuwa mashindano hayo ya siku tatu yataleta fahari kwa taasisi hiyo, ambayo imekusanya timu zilizofuzu […]

WAFANYABIASHARA ZAIDI YA 1,000 GITHURAI WAPOTEZA VIBANDA

Zaidi ya wafanyabiashara 1,000 katika Soko la Githurai wanakadiria hasara kubwa baada ya vibanda vyao kubomolewa alfajiri ya Alhamisi kupisha ujenzi wa kituo cha mabasi. Operesheni hiyo ilitekelezwa na Mamlaka ya Kitaifa ya Barabara Kuu Kenya (KENHA), siku moja tu baada ya wafanyabiashara hao kuandamana kupinga mpango wa ubomoaji. Ingawa walikuwa wamepewa notisi ya kuondoka, wamelalamikia […]

NDINDI NYORO AHOJI UUZAJI WA MALI ZA UMMA

Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro amesisitiza haja ya kuimarishwa kwa uwajibikaji wa kifedha, huku akipinga mpango wa serikali wa kubinafsisha Kampuni ya Kenya Pipeline na kuuza asilimia 15 ya hisa zake katika kampuni ya Safaricom. Akizungumza katika Kongamano la 34 la Kiuchumi lililofanyika jijini Nairobi, Nyoro ametaka serikali kuweka wazi maelezo kuhusu mpango wa uuzaji wa kampuni […]

FAMILIA ZADAI KUREJESHWA KWA  WAKENYA KUTOKA VITANI – URUSI

Familia za Wakenya waliorubuniwa kujiunga na jeshi la Urusi sasa zinaitaka serikali kuweka mpango maalum na wa haraka wa kuwarejesha wapendwa wao waliokwama katika eneo la vita. Jamaa wa waathiriwa hao, wanaodaiwa kuangukia mtego wa mtandao wa usafirishaji haramu wa watu, wamesema maombi yao ya mara kwa mara kwa idara husika hayajapatiwa uzito unaostahili. Takwimu […]

MURKOMEN AMJIBU VIKALI GACHAGUA

Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen amemjibu kwa ukali aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, akimtuhumu kwa siasa za kugawa wananchi kwa misingi ya kikabila na siasa za kiwango cha chini, huku akionya kuwa hatanyamaza tena. Akizungumza mjini Naivasha Murkomen amesema baadhi ya viongozi wa kisiasa wamejikita katika mashambulizi ya kibinafsi badala ya kuwasilisha sera […]

DUALE: WALIMU WANANUFAIKA NA SHA, POLISI KUFUATA APRILI

Waziri wa Afya Aden Duale amesema walimu tayari wanafaidi huduma za Mpango wa Afya wa Jamii, SHA, baada ya kujiunga na bima hiyo kuanzia mwezi Disemba. Akizungumza bungeni kuhusu bajeti ya wizara, Duale aMEsema maafisa wa polisi watajumuishwa katika mpango huo kuanzia mwezi Aprili mwaka huu. Waziri huyo ameeleza kuwa serikali imeokoa shilingi bilioni nane […]

MIKAKATI YA KEBS KUIMARISHA UDHIBITI WA UBORA WA BIDHAA ZINAZOAGIZWA

Shirika la kutathmini ubora wa biadhaa, KEBS, limetoa kandarasi kwa kampuni tisa za kimataifa kutekeleza huduma za uthibitishaji kabla ya mauzo ya nje ya ulinganifu (PVoC) kwa bidhaa za jumla zinazoingizwa nchini Kenya. Hatua hiyo inaanza kutekelezwa leo hii na itadumu kwa miaka mitatu. KEBS inalenga kuhakikisha bidhaa zinazoagizwa kutoka nje zinaafikia viwango vya soko la Kenya kabla ya kuondoka katika nchi za […]

MAWAKILI DEBENI KUWACHANGUA VIONGOZI WA LSK

Uchaguzi wa viongozi wapya wa chama cha wanasheria nchini LSK umeanza rasmi asubuhi, uchaguzi ambao huenda ukatoa mwelekeo mpya wa chama hicho. Mawakili wamejitokeza katika vituo vilivyoteuliwa vya kupigia kura, uchaguzi huo ukiandaliwa katika kipindi ambacho LSK imekuwa na nafasi kubwa katika kuhakikisha uongozi bora, uzingatiaji wa katiba na utawala wa sheria. Miongoni wanaowania wadhifa […]

ANTHONY GORDON AVUNJA REKODI YA SHEARER NEWCASTLE

Mshambulizi wa Newcastle United Anthony Gordon, alifunga mabao 4 jana usiku katika ushindi wa mabao 6-1 dhidi ta Qarabag ugenini nchini Azerbaijan, ukiwa ni ushindi mkubwa zaidi katika historia ya klabu hiyo ya Uingereza. Mabao hayo pia yalifikisha jumla ya mabao 10 kwa Mwingereza huyo, aliyevunja rekodi ya Allan Shearer na kuwa mchezaji ambaye ameifungia […]

GUNNERS WAPOTEZA SHABAHA EPL

Matumaini ya Arsenal kumaliza kiu cha miaka 20 cha kubeba taji la ligi kuu ya soka nchini Uingereza, EPL, yalipata pigo baada yao kupoteza uongozi wa mabao 2 na kuishia sare ya mabao 2-2 dhidi ya Wolves, timu ambayo tayari imekubali kushushwa daraja. Vijana hao wa Mikel Arteta walionekana kutamalaki mechi hiyo, wakichukua uongozi katika […]