ODM MBIONI KUOKOA CHOMBO
Chama cha ODM kimeratibiwa kuendelea na mkutano wake wa kamati ya utendaji hii leo katika kaunti ya Mombasa ambapo chama hicho kinalenga kuimarisha miundo ya kuzuia misukosuko inayotishia kukisambaratisha.
Mkutano huo unalenga kutathmini mikakati ya uhamasishaji katika kujiimarisha mashinani mbali na kujadili masuala yaliyoibuliwa kwenye vikao vya hivi punde vya ushirikishaji wa vijana katika kaunti kadhaa.
Mwenyekiti wa kitaifa Gladys Wanga, amekariri kuwa ODM ingali imara.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































