#Local News

KANG’ATA ABASHIRI MWANGUKO WA UDA

Gavana wa Murang’a Irungu Kang’ata amesema kuwa chama tawala cha UDA kimepoteza umaarufu katika eneo la Mlima Kenya, na kwamba kitaporomoka kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga, Kang’ata amesema mabadiliko ya kisiasa yanayoendelea yamesababisha chama hicho kupoteza umaarufu wake.

Kauli yake inajiri saa chache baada ya awali kutangaza kuwa hatawania muhula wa pili kwa chama cha UDA.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *