#Local News

GACHAGUA AMTETEA UHURU DHIDI YA SHUTUMA

Kinara wa chama cha DCP Rigathi Gachagua amemtetea Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta dhidi ya shutuma za viongozi wanaounga mkono serikali kuhusu msimamo wake kisiasa kama kinara wa chama cha Jubilee.

Akiwa kwenye ziara yake katika kaunti ya Kajiado, Gachagua amesisitiza kuwa Kenyatta ana haki kikatiba kutoa maoni yake kuhusu siasa za taifa, na uamuzi wa kumuunga mkono naibu wake Fred Matiang’i kama mgombeaji wa urais kwa chama cha Jubilee.

Hata hivyo, viongozi wa serikali wametishia kusimamisha marupurupu ya Kenyatta kama rais mstaafu iwapo ataendelea kujihusisha na siasa.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *