#Football #Sports

GOR MAHIA WAFUNGUA PENGO LA POINTI 9 KILELENI

Klabu ya Gor Mahia ilinufaika na bao la kujifunga kujipa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao Kakamega Homeboyz hapo jana, na kujiweka katika nafasi nzuri ya kunyakua taji la ligi kuu ya soka nchini, KPL kwa mara ya 22.

Kwenye mechi iliyoshuhudia ukame wa nafasi za ufungaji kutokana na nidhamu na tahadhari kutoka kwa timu zote, krosi ya Ebenezer Assifuah katika dakika ya 93 iliwalazimisha mabeki wa Homeboyz kufanya makosa, Peter Ng’ang’a akijifunga bao chini ya shinikizo.

Bao hilo lilitosha kuwapa K’Ogalo pointi zote 3, kwa sasa wakiwa na pointi 64, 9 mbele ya wapinzani wao AFC Leopards ambao wamekuwa wakisaka taji hilo kwa miaka 28 bila mafanikio.

Leopards wana mechi moja mkononi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *