MAHAKAMA YAAGIZA KUACHILIWA KWA MWAGODI MWABILI

Mahakama moja jijini Nairobi imetoa uamuzi wa pande mbili kuhusiana na maombi yaliyowasilishwa kuhusu uchunguzi na kuzuiliwa kwa mwanaharakati Mwagodi Mwabili. Katika ombi la kwanza, mahakama iliruhusu Idara ya Upelelezi wa Jinai kuendelea kushikilia simu ya mkononi ya Mwabili kwa ajili ya uchunguzi zaidi, ikisema kifaa hicho ni muhimu kama kielelezo katika uchunguzi wa machapisho […]

SIFUNA APINGA MKATABA WA USHIRIKIANO KATI YA KAUNTI NA SERIKALI KUU

Seneta wa Kaunti ya Nairobi Edwin Sifuna amemtaka Gavana Johnson Sakaja kufutilia mbali mkataba aliotia sahihi na serikali kuu kuhusu ushirikiano wa utendakazi wa kaunti. Sifuna amesema makubaliano hayo ni kinyume cha sheria na ameahidi kuongoza pingamizi dhidi yake hadi mahakamani. Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino naye ameungana na Sifuna, akisema mkataba huo wa […]

RAIS RUTO NA SAKAJA WAZURU SEHEMU ZA NAIROBI

Rais William Ruto na Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja wamezuru maeneo kadhaa katika kaunti ya Nairobi, siku moja baada ya Serikali ya Kaunti ya Nairobi na Serikali Kuu kutangaza makubaliano ya kushirikiana katika sekta nne za maendeleo. Ziara hiyo imelenga kukagua hali halisi ya maeneo yatakayoguswa na miradi hiyo ya maendeleo. Rais Ruto anaendelea na ziara […]

MAHAKAMA KUU YAPOKEA OMBI LA KUPINGA MKATABA WA USHIRIKIANO

Ombi la kikatiba linalopinga uhalali wa Mkataba wa Ushirikiano kati ya Serikali ya Kitaifa na Serikali ya Kaunti ya Jiji la Nairobi limewasilishwa katika Mahakama Kuu. Jaji Bahati Mwamuye amelitambua ombi hilo lililowasilishwa na Christine Gathoni pamoja na Benard Peter kuwa la dharura akibaini kuwa Notisi ya Hoja ya waombaji inaibua maswali kuhusu uhalali na ulinganifu wa […]

MABABE WA ULAYA WAFUFUA MATUMAINI

Miamba wa soka barani Ulaya wakiwemo mabingwa watetezi wa dimba la klabu bingwa barani humo PSG, Real Madrid, na Borussia Dortmund waliweka hai matumaini ya kufuzu raundi ya 16 za mwisho baada ya kuandikisha ushindi katika mkondo wa kwanza wa mechi za mwondoano. Real walipata ushindi mwembamba wa goli moja ugenini dhidi ya Benfica yake […]

MIAMBA WA AFRIKA KUMENYANA ROBO FAINALI CAF CL

Bingwa wa kihistoria mara 12 wa taji la klabu bingwa barani Afrika CAF Champions League, Al Ahly wa Misri, watakabiliana na Esperance Sportive de Tunis wa Tunisisa katika pambano la wazito wa Kaskazini mwa Afrika kwenye awamu ya robo fainali ya ubingwa huo. Hii ni kulingana na droo iliyofanywa hapo jana nchini Misri, ambapo Al […]

DROO YA ROBO FAINALI CAF CONFEDERATIONS CUP

Debi la Morocco ndilo gumzo kubwa katika awamu ya robo fainali ya dimba la mashirikisho, CAF Confederations Cup msimu wa 2025-26, kufuatia droo iliyofanyika hapo jana nchini Misri. Olympique de Safi watakuwa wenyeji Wydad Casablanca kwenye mkondo wa kwanza wa robo fainali hiyo, katika pambano la timu zinazofahamiana vyema na litakalohakikisha kuwa Morocco ina mwakilishi […]

AZMA YA GSU LIGI YA KVF INAPORUDI

Klabu ya voliboli ya GSU inaazimia kuweka nyuma masaibu yao katika ligi ya wanaume ya mchezo huo inayorejelewa hapo kesho ugani Kasarani Indoor Arena. Mabingwa hao watetezi walikuwa na mwanzo duni, wakikosa kuandikisha ushindi katika mechi zao 2 za mkondo wa kwanza, ila kocha mkuu Gideon Tarus amesema wana matumaini ya kujikung’uta vumbi na kuwaonyesha […]

WAKAZI WASHINIKIZA MWANGA UREJEE WEBUYE

Wakazi na wafanyibiashara katika eneo la Dina mjini Webuye wamelalamikia kukithiri kwa visa vya uhalifu, hali wanayodai imechangiwa na kuharibika kwa taa za barabarani yaani Mulika Mwizi, eneo hilo Wakizungumza baada ya kuhudhuria mkutano wa kufunguliwa tena kwa vyoo vya soko la Dina vilivyokuwa vimefungwa kwa muda, wakaazi hao wamesema kuwa wanapitia changamoto kuendeleza shughuli zao za kawaida kutokana na giza, […]

MAFURIKO YATATIZA USAFIRI NAIROBI

Shughuli za kawaida zimerejelewa kwenye barabara za Kangundo na Eastern Bypass jijini Nairobi baada ya watumizi kutazika usiku kucha kutokana na mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha mafuriko kwenye barabara hizo. Wakazi wamesema chanzo cha mafuriko hayo kwenye mikondo ya maji ni hali duni ya miundomsingi katika kaunti ya Nairobi, ambayo husababisha mafuriko kila mvua inaponyesha. […]