DROO YA FA CUP

Jumla ya timu 14 zimefuzu Raundi ya 5 ya dimba la FA Cup nchini Uingereza, zikisubiri kwa hamu kufahamu wapinzani wao katika droo itakayoandaliwa leo usiku kabla ya mechi kati ya Brentford na Macclesfield. Awamu ya 5 ni wazi, ikiwa na maana kwamba timu inaweza kupewa mpinzani kutoka ligi yoyote bila vikwazo. Miongoni mwa wanaosubiri […]

GOR WAPANUA PENGO LA ALAMA, INGWE WASHIKWA

Mabingwa mara 21 wa ligi kuu ya soka nchini, KPL, Gor Mahia, waliongeza pengo la alama kwenye uongozi wa ligi hiyo hadi pointi 6 kufuatia ushindi mwembamba wa mabao 2-1 dhidi ya APS Bomet ugani Green Stadium mjini Kericho hapo jana. Ushindi huo ukijiri baada ya washindani wao AFC Leopards kukatwa kucha tena na Bandari […]

SHUJAA WATANGAZA USHUJAA WORLD RUGBY SVNS

Kikosi cha taifa cha raga cha wanaume Kenya Sevens maarufu kama Shujaa, kiliwika nyumbani kwa kuandikisha ushindi mara 4 kati ya 5 katika mkondo wa kwanza wa mashindano ya HSBC World Rugby Sevens Division 2, na kumaliza katika nafasi ya tatu kwa msimamo wa jumla katika uwanja wa Nyayo hapo jana. Katika mashindano hayo yaliyopewa […]

NDOTO YA RISINGI STARLETS FIFA U20 YAZIMWA

Safari ya kikosi cha chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 Rising Starlets kushiriki dimba la kombe la dunia mwaka huu nchini Poland ilitamatika Jumamosi ugenini dhidi ya Tanzania, baada ya chipukizi hao wa Jackline Juma kupoteza uongozi wa bao 1-0 kutoka mkondo wa kwanza. Uongozi waliobeba kuelekea mkondo wa pili uliwaponyoka katika dakika ya 70 […]

MIMI NDIO SIFUNA KITENGELA!

Viongozi wa chama cha ODM wanaoegemea mrengo wa katibu mkuu Edwin Sifuna wametangaza kumuunga mkono Sifuna kupinga ushirikiano wa kisiasa kati ya ODM na chama tawala cha UDA kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka ujao. Viongozi hao akiwemo naibu kinara Godfrey Osotsi ambaye ni seneta wa Vihiga, gavana wa Siaya James Orengo na mbunge wa […]

ASIMILIA 70 YA VITABU IMESAMBAZWA, SERIKALI

Jumla ya vitabu milioni 8.35 vya gredi ya 10 vimesambazwa katika shule za umma za sekondari ya juu kufanikisha masomo ya kiwango hicho chini ya mtaala wa umilisi CBE, huku vitabu vilivyosalia vikiratibiwa kusambazwa kufikia mwishoni mwa mwezi huu. Kupitia taarifa, wizara ya elimu imesema zoezi hilo la usambazaji kote nchini, linaendelea huku vitabu vilivyosambazwa […]

GACHAGUA ASISITIZA RUTO HARUDI MADARAKANI

Kinara wa chama cha DCP Rigathi Gachagua amepuzilia mbali mjadala unaoendelea kuhusu wadhifa wa atakayekuwa naibu wa Rais William Ruto kwenye muhula ujao kati ya naibu wa sasa Kithure Kindiki na mwanachama wa ODM, akisema Ruto hatapata muhula wa pili. Kwa mujibu wa Gachagua, muungano wa upinzani unafanya kila uwezalo kuhakikisha kuwa Rais Ruto anahudumu […]

KINDIKI: KITI CHANGU NI CHANGU

Mjadala kuhusu ni nani atakayekuwa naibu wa Rais William Ruto kwenye uchaguzi mkuu ujao umeendelea kushika kasi, naibu Rais Kithure Kindiki akisisitiza kuwa kamwe hatawachia wadhifa huo. Akizungumza katika eneo la Imenti kaunti ya Meru, Kindiki amewahakikishia wafuasi wake kwamba wadhifa huo ungali chini yake hadi muhula wa pili wa Rais Ruto madarakani, na kwamba […]

Insider Secrets to Better Odds on European Roulette at Big Win

Insider Secrets to Better Odds on European Roulette at Big Win European roulette is the go‑to wheel for players who want the best chance to win. While the game looks simple, the little details can make a big difference in your bankroll. In this guide we’ll walk through the typical problems players face, explain why […]

ARSENAL WANAENDELEA KUANGALIA TAJI, SIO MANCHESTER CITY

Kiungo wa Arsenal, Declan Rice, amesema timu yake haiwezi kuzingatia tuzungumzo kuhusu Manchester City kufuata karibu kileleni mwa Ligi Kuu baada ya Gunners kucheza 1-1 na Brentford Alhamisi. City sasa wako pointi 4 nyuma ya Arsenal na watakuwa na faida ya uwanja wakati pande hizo zinakutana Aprili. Arsenal inatarajia kumaliza safari ya miaka 22 bila […]