SIKU YA KIHISTORIA GRADE 10

Pilkapilka za kujiunga na gredi ya 10 katika shule za sekondari ya juu zimeshika kasi huku kundi hilo la kwanza likianza safari yao hii leo chini ya mtaala wa umilisi CBE. Wengi wa wazazi wamelalamikia muda mfupi waliopewa na wizara ya elimu kujiandaa, hatua ambayo imesababisha misongamano kwenye maduka ya kuuza bidhaa za shule. Wakati […]

GACHAGUA ASISITIZA KAULI ZAKE

Aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua amesisitiza haja ya kila eneo nchini kuimarisha miundomsingi yake ili kuboresha utoaji huduma kwa wananchi ikiwemo shule na kupunguza hulka za Watoto kulazimika kusomea shule za mbali. Akizungumza katika eneo la Gatundu kaunti ya Kiambu, Gachagua amekariri msimamo wake kwamba wanafunzi wanapaswa kupewa nafasi katika shule zilizo karibu na wanakotoka. […]

RUTO: NITAWATIMIZIA KABLA YA KUWAOMBA TENA

Rais William Ruto amewahakikishia wakazi wa Mlima Kenya kwamba atakamilisha ahadi zote alizotoa kwao kwenye kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu uliopita kabla ya kuwaomba kura za muhula wa pili. Rais alikuwa akizungumza katika eneo bunge la Othaya akiwa kwenye ziara yake ya siku 3 katika eneo la Mlima Kenya, ambako amewataka wakazi kuwatathmini viongozi kutokana […]

TSC YASEMA TAYARI KWA GRADE 10

Tume ya kuwaajiri walimu TSC imewahakikishia wazazi na washikadau wa elimu kwamba taifa limejiandaa kikamilifu kwa mpito wa masomo ya gredi ya 10, ikisema walimu wamepewa mafunzo kikamilifu kushughulikia masomo hayo. Akizungumza jijini Eldoret wakati wa kutangazw kwa matokeo ya KCSE yam waka 2025, afisa mkuu mtendaji wa TSC Eveleen Mitei, amesema walimu wote wameandaliwa […]

KNEC: THIBITISHA USAJILI WA MWANAO

Baraza la mitihani ya kitaifa KNEC limewataka wazazi kuthibitisha kwamba wanao wamesajiliwa kwenye mitihani ya kitaifa ya gredi ya 6, 8 na kidato cha 4 kwa kutumia mfumo wa ujumbe mfupi wa maandishi SMS utakaotumika kuanzia Aprili mwaka huu. Afisa mkuu mtendaji wa KNEC David Njeng’ere, amesema hilo litapunguza changamoto za watahiniwa kukosa kukalia mitihani […]

KCSE 2025: WATAHINIWA 1,180 WAKOSA MATOKEO

Huku sherehe zikiendelea kuhusiana na matokeo ya mtihani wa KCSE mwaka 2025, watahiniwa 1,180 hawana cha kufurahia baada ya wizara ya elimu kufutilia mbali matokeo yao kwa madai ya kuhusika na udanganyifu kwenye mtihani huo. Akizungumza katika shule ya AIC Chebisas kaunti ya Uasin Gishu wakati wa kutangaza matokeo hayo, Waziri wa elimu Julius Ogamba […]

KCSE 2025: IDADI YA A PLAIN YAONGEZEKA

Jumla ya watahiniwa 1,932 wa mtihani wa KCSE mwaka jana walipata alama ya A plain kwenye mtihani huo, ikiwa ni ongezeko la gredi hiyo ikilinganishwa na watahiniwa 1,693 waliopata A plain mwaka 2024. Haya ni kulingana na matokeo ya mtihani wa KCSE 2025 ambayo yametangazwa na Waziri wa elimu Julius Ogamba, akisema idadi ya watahiniwa […]

1,932 WAPATA A KCSE 2025

Watahiniwa 270,000 wa mtihani wa KCSE wa mwaka jana wamepata alama ya C+ na zaidi, ambayo ni alama ya wastani ya kuijunga na vyuo vikuu, ambayo ni asilimia 27 ya watahiniwa 993,000 waliokalia mtihani huo wa mwaka jana. Akizungumza baada ya kukabidhiwa matokeo hayo katika Ikulu ndogo ya Eldoret, Rais William Ruto ameweka wazi kwamba […]

ARSENAL WAPOTEZA NAFASI YA KIPEKEE

Viongozi wa ligii ya soka nchini Uingereza, EPL, Arsenal, walipoteza nafasi ya kupanua mwanya wa pointi 8 uongozini mwa ligi hiyo baada ya kutoa sare ya kutofungana dhidi ya Liverpool ugani Emirates Stadium. The reds ni mojawapo ya timu 2 pekee ambazo zimefanikiwa kuwacharaza vijana wa Mikel Arteta msimu huu, na walikaribia kuikabidhi kichapo cha […]

ROBO FAINALI ZA AFCON KUANZA LEO

Robo fainali za Kombe la Mataifa bingwa barani Afrika, AFCON, zinaanza leo huku mataifa 8 yakipigania nafasi ya kutinga nusu fainali. Algeria itavaana na Nigeria katika mechi kali, Algeria ikiwa haijapoteza mchezo wowote kwenye mashindano haya na inajivunia safu imara ya ulinzi. Nigeria, kwa upande wake, ina moja ya safu kali zaidi za ushambuliaji, ikiwa miongoni mwa timu zilizofunga mabao mengi zaidi hadi sasa.na ina rekodi nzuri katika […]