AK YASIFU TIMU YA KENYA BAADA YA MAFANIKIO MAKUBWA DUNIANI

Shirikisho la Riadha Kenya (AK) limesifu Timu ya Kenya kwa maonyesho ya kuvutia na uwakilishi bora wa taifa katika Mashindano ya 46 ya Dunia ya Mbio za Nyika. Timu ya Kenya inatarajiwa kurejea nchini baada ya kung’ara katika mashindano hayo yaliyofanyika Jumamosi mjini Tallahassee, Florida, Marekani. Kenya iliongoza jedwali la medali kwa mara ya tatu […]

XABI ALONSO AACHANA NA REAL MADRID, ARBELOA ATEULIWA KOCHA MPYA

Klabu ya Real Madrid imetangaza kwamba kocha Xabi Alonso ameondoka katika klabu hiyo kwa makubaliano ya pande zote, huku nafasi yake ikichukuliwa na Alvaro Arbeloa. Tangazo hilo lilikuja siku moja baada ya Real Madrid kupoteza fainali ya Kombe la Super Cup la Uhispania kwa Barcelona. Baada ya kipigo hicho, mabingwa hao wa zamani wa Ulaya […]

HOWE APINGA MABADILIKO YA KANUNI ANAPOJIANDAA KWA CITY

Kocha wa Newcastle United, Eddie Howe, amekiri kuwa hangeunga mkono mabadiliko ya kanuni yaliyowezesha timu yake kukutana na Antoine Semenyo wakati watakapocheza dhidi ya Manchester City leo usiku katika mkondo wa kwanza wa mechi ya semi fainali ya Carabao Cup. Mabingwa hao watetezi wa Kombe la Carabao wanakabiliwa na mtihani mgumu hadi sasa katika jitihada zao za kutetea […]

CAF YAFUNGUA UCHUNGUZI BAADA YA VURUGU KATI YA ALGERIA, NIGERIA

Shirikisho la Soka barani Afrika, CAF, limetangaza kuwa limefungua uchunguzi na kuonya juu ya uwezekano wa kuchukua hatua za kinidhamu kufuatia tabia iliyoelezwa kuwa isiyokubalika baada ya wachezaji wa Algeria na Nigeria kukabiliana uwanjani mwishoni mwa mechi yao ya robo fainali ya Kombe la Mataifa bingwa ya Afrika, AFCON. Mvutano ulizuka uwanjani baada ya kipenga cha mwisho cha mechi ya Jumamosi iliyochezwa mjini Marrakesh, […]

KPL: AMBANI AAMINI AFC LEOPARDS TAYARI KUPIGANIA UBINGWA WA LIGI

Kocha mkuu wa AFC Leopards, Fred Ambani, amesema ana imani kubwa kuwa kikosi chake kiko tayari kutoa ushindani wa kweli katika mbio za kutwaa taji la Ligi Kuu ya Kenya, KPL, msimu huu. Ambani, ambaye alikuwa miongoni mwa kikosi kilichotwaa ubingwa wa mwisho wa ligi wa klabu hiyo mwaka 1998 pamoja na ndugu yake na mwenyekiti wa sasa wa […]

OGAMBA AONYA DHIDI YA SIASA SHULENI

Waziri wa Elimu Julius Ogamba amewaonya viongozi wa kisiasa dhidi ya kuingiza siasa katika masuala ya elimu, akisema hulka hizo zinaibua hofu miongoni mwa wazazi na wanafunzi nchini. Akizungumza katika kaunti ya Murang’a, Ogamba amerejelea kauli ya aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua kwamba wanafunzi wajiunge na shule za kitaifa zilizo katika maeneo wanakotoka, akisisitiza kuwa […]

ODM YAANDAA NDOA NA UDA

Kamati kuu ya chama cha ODM imeidhinisha kuanzishwa mara moja kwa mazungumzo mara na chama tawala cha UDA kuhusu kubuniwa kwa muungano wa kisiasa baina ya vyama hivyo kuelekea uchaguzi mkuu ujao. Akizungumza baada ya mkutano wa kamati hiyo kaunti ya Kilifi, kinara wa chama hicho Oburu Oginga, amesema makubaliano ya vyama hivyo yataidhinishwa na […]

OGAMBA: KUNA NAFASI YA KUBADILISHA SHULE

Wazazi walio wa wanafunzi wanaojiunga na gredi ya 10 wamepewa hakikisho kwamba wangali na nafasi ya kubadilisha shule walizowekwa wanao, baada ya kuibuka kwamba baadhi ya wanafunzi wamewekwa katika shule za jinsia tofauti. Hakikisho hilo limetolewa na Waziri wa Elimu Julius Ogamba, huku zoezi la kuwapokea wanafunzi hao likiingia siku ya pili hii leo baada […]

JSC YAENDELEZA MSAKO WA MAJAJI

Mwenyekiti wa mamlaka ya kuangazia utendakazi wa polisi IPOA Issak Hassan na mchanganuzi wa masuala ya kikatiba Prof Migai Aketch, ni miongoni mwa wawaniaji wanaotaka kuteuliwa kama majaji wa mahakama ya rufaa kwenye mchakato unaoendelea wa kuwateua majaji wa mahakama hiyo na mahakama kuu. Akizungumza mbele ya jopokazi la uteuzi la tume ya JSC, Hassan […]

HATIA MASHIRIKA YA UMMA KUTUMIA HUDUMA ZA BINAFSI- MAHAKAMA

Mahakama kuu imetoa amri za muda kuzuia mashirika ya umma kuwakilishwa mahakamani na mawakili binafsi hadi kesi ya kikatiba iliyowasilishwa na seneta wa Busia Okiya Omtatah, mkenya kwa jina Dakta Benjamin Magare na wengine itakaposikilizwa na kuamuliwa. Katika uamuzi huo, mahakama aidha imemwagiza mdhibiti wa bajeti ya serikali kutoidhinisha malipo yoyote kwa mawakili wasio wa […]