JUNET: UPINZANI UNAWEZA KUMUUNGA MKONO RUTO 2027

Mbunge wa Suna East, Junet Mohamed, ameashiria mabadiliko ya kisiasa yanayoweza kutokea akisema upinzani unaweza kumuunga mkono Rais William Ruto katika Uchaguzi Mkuu wa 2027 iwapo mazungumzo yanayoendelea yatazaa matunda chanya. Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha runinga humu nchini, Junet alieleza kuwa siasa hazitabiriki na akasisitiza kuwa hakuna chaguo lililoondolewa mezani. Mbunge huyo alikuwa […]

OGAMBA AFAFANUA: WANAFUNZI WA SHULE ZA C4 HAWALIPI KARO

Waziri wa Elimu, Julius Ogamba, amefafanua kuwa wanafunzi waliowekwa katika shule za C4 hawatakiwa kulipa karo yoyote, huku serikali ikiongeza jitihada za kuhakikisha mpito kamili wa wanafunzi hadi shule za sekondari ya juu chini ya Mtaala wa Umahiri (CBC). Shule za C4 zinatambulika kama shule za siku za kaunti ndogo chini ya makundi yaliyorekebishwa ya shule za […]

VIFO VYA ZAIDI YA 290 VIMERIPOTIWA JANUARI 2026, TAKWIMU ZA POLISI

Zaidi ya watu 290 wamefariki katika siku 21 za mwanzo wa Januari 2026, kulingana na takwimu zilizokusanywa na polisi. Hapo jana watu saba waliuawa katika ajali tofauti nchini, na kuongeza idadi ya vifo hadi 294 katika siku 21 miongoni mwao wakiwa ni Pamoja na watembea miguu wawili, abiria wawili, waendesha pikipiki wawili, na abiria wa pikipiki mmoja. Polisi wamesema […]

MAAFISA WA SERIKALI KUSIMAMIA UHAMISHO WA WANAFUNZI HADI GREDI YA 10

Maafisa wa Utawala wa Serikali ya Kitaifa  sasa wataongoza ufuatiliaji katika maeneo ya makazi ili kuhakikisha asilimia 100 ya wanafunzi wanahamia Gredi ya 10. Waziri wa Usalama wa Ndani, Kipchumba Murkomen, amesema serikali inachukua mkakati wa ushirikiano ili kusaidia wanafunzi wasio na uwezo wa kulipa karo akieleza kuwa wanafunzi hao watabainishwa kupitia maafisa wa NGAO na kuelekezwa […]

MIANO ATAKA KAUNTI KUIMARISHA FURSA ZA UTALII

Waziri wa Utalii na Wanyamapori, Rebecca Miano, amezitaka serikali za kaunti kubaini, kuendeleza na kutangaza kikamilifu fursa mbalimbali za utalii katika maeneo yao ili kusaidia Kenya kufikia malengo yake ya ukuaji wa sekta hiyo. Akizungumza mjini Naivasha, Miano alisisitiza kuwa sekta ya utalii inahitaji ushirikiano wa karibu ili kufikia uwezo wake kamili akisema Kenya inalenga kuvutia […]

HUDUMA ZA AFYA ZATATIZIKA HOSPITALI YA MAMA LUCY

Huduma za afya katika hospitali ya mama Lucy katika kaunti ya Nairobi zimetatizika kufuatia mgomo wa matabibu na madaktari wa Kaunti huku madaktari wanafunzi wakiachwa kushughulikia Wagonjwa. Chama cha matabibu nchini kimesisitiza kuwa wanachama wake hawatarudi kazini hadi pale madai yao yatakaposikilizwa na Serikali ambayo ni Pamoja na kulipwa kwa malimbikizi ya mishahara ya miezi […]

MURKOMEN: SERIKALI ITACHUKUA HATUA KALI DHIDI YA UKATILI WA POLISI

Waziri wa Usalama wa Ndani, Kipchumba Murkomen, amesema visa vya hivi karibuni vya ukatili wa polisi vilivyoripotiwa katika maeneo mbalimbali ya nchi vimechochea mazungumzo mapya na makamanda wa polisi ili kudhibiti mienendo mibaya na kurejesha imani ya umma kwa vyombo vya usalama. Akizungumza mjini Kisumu, Murkomen amewahakikishia Wakenya kuwa serikali itachukua hatua kali dhidi ya […]

MZOZO WA ARDHI TRANSMARA

Wanakijiji   katika mpaka wa Transmara na Migori wanalilia serikali kuwanusuru dhidi ya watu  walio na lengo la kuwafurusha katika makao yao  kwa njia ya mkato. Wenyeji hao   wanadai kuhangaishwa na wanaomezea mate ardhi hiyo huku wakidai zaidi ya vijana 15 wakikamatwa kiholela kufuatia mzozo wa mara kwa mara kuhusu mashamba yaliyoko katika mpaka huo. Sasa wanaomba maafisa wakuu […]

RUKU AWAHAKIKISHIA WAKAZI WA TANA RIVER MSAADA WA SERIKALI

Waziri wa utumishi wa umma  Geoffrey Ruku amewahakikishia wakazi wa kaunti ya Tana river ahadi ya serikali ya kusaidia familia zilizoathiriwa na hali mbaya ya ukame . Akizungumza wakati wa usambazaji wa chakula cha msaada, waziri huyo amesema serikali inafanya kazi kusaidia familia 180 . Ruku amebainisha kuwa utoaji wa chakula cha msaada umehitajika kutokana na ukame unaoendelea, na kuziacha familia nyingi […]

WAHALIFU WAWILI WAKAMATWA KISUMU

Wanaume wawili wamekamatwa Kisumu baada ya polisi kupata silaha na vitu vinavyoaminika kutumika katika shughuli za  uhalifu . Katika taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wa  x  , polisi wamesema watu hao   walikamatwa kwenye kivuko cha reli huku wakidaiwa kujiandaa kufanya uhalifu katika eneo hilo. Operesheni hiyo ilizinduliwa baada ya wakazi kutoa tahadhari kuhusu mienendo yenye mashaka karibu na barabara yenye shughuli nyingi, […]