ERIC OUMA KARIBU KUREJEA UWANJANI

Mchezaji wa Harambee Stars, Eric Ouma maarufu kama ‘Marcelo’, yuko karibu kurejea uwanjani baada ya miezi tisa, akiwa na klabu yake ya Raków Częstochowa nchini Poland. Mlinzi huyo wa kushoto mwenye umri wa miaka 29 alipata jeraha la kupasuka kwa kano la kisigino wakati wa mazoezi Agosti 28, 2025, jambo lililomwathiri pakubwa katika msimu wa […]

AMBANI AFURAHISHWA NA USHINDI WA LEOPARDS

Kocha wa AFC Leopards, Fred Ambani, ameonyesha kuridhishwa na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Murang’a Seal katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa Uwanja wa Nyayo. Matokeo hayo yameimarisha mbio za ubingwa kwa Leopards, yakipunguza tofauti ya pointi kati yao na vinara wa ligi, Gor Mahia, hadi pointi mbili baada ya michezo 27 ya msimu. […]

NAIROBI CITY THUNDER WAMALIZA MASHINDANO YA AFRIKA KWA USHINDI

Derrick Ogechi alifunga pointi 22 na kuiongoza Nairobi City Thunder kumaliza mashindano ya Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika kwa ushindi, baada ya kuwashinda RSSB Tigers ya Rwanda kwa mara ya kwanza katika michuano hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa SunBet Arena. City Thunder, waliomaliza na ushindi wa michezo miwili na kupoteza mitatu, waliibuka na ushindi […]

MAWAZIRI WACHUNGUZWA KATIKA SAKATA YA MAFUTA

Mawaziri wawili ni miongoni mwa wanaochunguzwa kuhusiana na sakata ya mafuta ya shilingi bilioni 4.8 iliyosababisha kukamatwa na kujiuzulu kwa wakuu watatu wa sekta ya kawi. Sakata hiyo inahusisha uingizaji wa shehena mbili za petroli zenye uzito wa tani 128,000 nje ya makubaliano ya kiserikali ya ununuzi wa moja kwa moja, ambapo serikali hununua mafuta […]

ATANDI APINGA HOJA YA KUMWONDOA ORENGO

Mbunge wa Alego Usonga, Samuel Atandi, amepinga wito unaoendelea wa kumwondoa madarakani Gavana wa Siaya, James Orengo, akisema hatua hiyo si ya lazima wakati uchaguzi mkuu ujao ukiwa umesalia muda mfupi. Atandi amesema hatashiriki mjadala wa kumwondoa Orengo, akisisitiza kuwa badala yake gavana huyo anapaswa kupingwa kupitia kura katika uchaguzi. Mbunge huyo ameeleza kuwa hakuna […]

OLEKINA AONYESHA NIA YA NAFASI ODM

Seneta wa Narok, Ledama Olekina, ametangaza utayari wake wa kuchukua wadhifa wa Katibu Mkuu wa Chama cha ODM. Haya yanajiri wakati chama hicho kinaendelea na hatua za kinidhamu dhidi ya anayeshikilia wadhifa huo kwa sasa, Edwin Sifuna. Akizungumza katika mahojiano, Olekina amepuuza taarifa kuwa amependekezwa rasmi kwa nafasi hiyo, lakini akasisitiza kuwa hatasita kuchukua jukumu hilo akipewa […]

DUALE AJIBU GACHAGUA KUHUSU SHA

Waziri wa Afya, Aden Duale, amesema hatakatishwa katika juhudi zake za kutekeleza majukumu yake, huku mvutano ukizidi kati yake na aliyekuwa Naibu Rais, Rigathi Gachagua, kuhusu usimamizi wa mamlaka ya afya ya jamii (SHA). Akizungumza mjini Garissa, Duale amekanusha madai ya Gachagua kwamba anahusika na ufisadi katika mfumo wa bima ya afya chini ya mpango […]

UHABA WA MAFUTA WAKUMBA KAKAMEGA

Madereva katika mji wa Kakamega wanakabiliwa na uhaba wa mafuta uliosababisha usumbufu mkubwa katika usafiri na shughuli za kila siku. Kwa mujibu wa baadhi ya madereva, vituo vingi vya mafuta mjini humo vimeishiwa na mafuta, huku ni vituo viwili pekee vinavyoripotiwa kuwa bado vina akiba, hali ambayo imelazimisha madereva kusafiri umbali mrefu kutafuta mafuta, huku baadhi […]

LIAM ROSENIOR ASEMA UHUSIANO NA FERNANDEZ UKO VIZURI

Kocha wa Chelsea Liam Rosenior amesisitiza kuwa uhusiano wake na kiungo wa Enzo Fernandez wa Chelsea uko “vizuri” licha ya uamuzi wa kumfungia Fernandez michezo miwili. Kocha huyo wa Blues aliamua kumfungia Fernandez mchezo wa Jumamosi wa ushindi wa 7-0 dhidi ya Port Vale katika robo fainali ya Kombe la FA, baada ya Fernandez kuashiria kuwa angekuwa tayari […]

VIRGIL VAN DIJK AOMBA RADHI MASHABIKI WA LIVERPOOL

Virgil Van Dijk amewaomba radhi mashabiki wa Liverpool baada ya kukiri kuwa timu yake ilikata tamaa katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la FA dhidi ya Manchester City. Timu ya Arne Slot ilipoteza 4-0 katika Uwanja wa Etihad Jumamosi, jambo lililomfanya Van Dijk kuchukizwa na kiwango cha nusu ya pili. Liverpool walikuwa nyuma 2-0 […]