TUJU AACHILIWA KWA DHAMANA

Aliyekuwa waziri Raphael Tuju amefikishwa katika mahakama ya Kibera akikabiliwa na shtaka la kutoa taarifa za uongo kwa afisa wa polisi. Inadaiwa kuwa Tuju aliripoti tukio la kutekwa nyara katika eneo la Karen jijini Nairobi tarehe mosi Machi taarifa ambayo upande wa mashtaka unasema haikuwa ya kweli. Tuju amekanusha shtaka hilo na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi […]

RAIS AIDHINISHA BAJETI YA ZIADA

Rais William Ruto ameidhinisha mswada wa matumizi ya ziada wa mwaka 2026, hatua inayoruhusu ongezeko la matumizi ya serikali ya shilingi bilioni mia tatu sitini na tatu, zaidi ya pendekezo la awali la hazina. Hafla ya utiaji saini ilifanyika katika Ikulu, huku kukiwa na wasiwasi unaoongezeka kuhusu deni la taifa na usimamizi wa fedha za […]

KRA YAPATA SH17.6BN KUONGEZA UKUSANYAJI WA USHURU

Serikali imetenga Sh17.6 bilioni za ziada kwa Mamlaka ya Ushuru (KRA) ili kuimarisha ukusanyaji wa ushuru na kupunguza utegemezi wa kukopa kwa umma. Ufadhili huo ni sehemu ya Makadirio ya Ziada ya I kwa mwaka wa kifedha wa 2025/2026, yaliyoidhinishwa na Rais William Ruto.Mgao huo unajiri huku KRA ikilenga kukusanya takriban Sh900 bilioni kufikia Juni 2026 ili […]

UCL: BAYERN WAVUNA UGENINI, HAVERTZ AIPA ARSENAL NAFUU YA JIONI

Luiz Diaz na Harry Kane walifunga mabao mawili na kuipa ushindi timu yao ya Bayern Munich ugenini dhidi ya Real Madrid katika mechi ya awamu ya robo fainali ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya jana usiku. Baada ya kutamalaki kwa kipindi kirefu na kuendeleza mashambulizi ya mara kwa mara, Diaz alifungua ufungaji wa […]

FIFA U17 WC: STARLETS WAJIANDAA MAZOEZINI

Kikosi cha chipukizi wa timu ya taifa ya soka ya wanawake Junior Starlets kimeimarisha mazoezi yake kinapojiandaa kwa mechi ya kufuzu mashindano ya FIFA U17dhidi ya Namibia, kinapolenga kurejea katika mashindano hayo ya kimataifa. Kikosi hicho kilichofanya mazoezi yake katika uwanja wa Kasarani jana, kitachuana na Namibia kwenye mikondo miwili, tarehe 12 na marudiano tarehe […]

KENYA YAKABILIWA NA UHABA WA MAFUTA

Kenya inakabiliwa na uhaba wa mafuta ambao huenda ukaathiri uchukuzi, madereva wakiripoti ugumu wa kupata bidhaa hiyo licha ya serikali kusisitiza kuwa taifa lina akiba ya kutosha. Miongoni mwa maeneo ambako foleni ndefu zimeshuhudiwa katika vituo vya kuuza mafuta ni Magharibi mwa nchi, Kisii na bonde la ufa. Wameitaka serikali kuweka wazi hali halisi ya […]

GACHAGUA: DCI HAIWEZI KUJICHUNGUZA

Idara ya upelelezi wa jinai DCI imetakiwa kujiondoa kwenye uchunguzi unaoendelea katika Sakata ya mafuta iliyosababisha kupotea kwa shilingi bilioni 2.9, kwa misingi kwamba ilihusika katika uagizaji wa mafuta hayo. Kiongozi wa chama cha DCP Rigathi Gachagua, amesisitiza kwamba idara hiyo ni mwanachama wa kamati ya kitaifa ya usalama, NSAC, na hivyo itavuruga uchunguzi huo […]

WANDAYI, ONE PETROLEUM WAVUTANA KUHUSU MAFUTA

Vuta nikuvute imeibuka baina ya wizara ya kawi na kampuni ya One Petroleum iliyoagiza tani 60,000 za pteroli, baada ya waziri wa kawi Opiyo Wandayi kuagiza kwamba shehena hiyo irejeshwe ilikotoka. Hata hivyo, kampuni hiyo imepinga amri ya Wandayi, ikisema ilishinda kihalali tenda ya uagizaji mafuta, ikiwa ni miongoni mwa kampuni 4 zilizopewa tenda hiyo […]

MSHUKIWA WA ‘ASIDI’ KUENDELEA KUZUILIWA

Mshukiwa anayekabiliwa na mashtaka ya kumshambulia mwanamke kwa kummwagia asidi anataendelea kuzuiliwa kwa siku 5 zaidi ili kuwaruhusu wapelelezi kukamilisha uchunguzi dhidi yake. Hii ni baada ya mshukiwa huyo kwa jina Elvis Opiyo kukana mashtaka dhidi yake alipofikishwa katika mahakama kuu ya Kibra, kesi hiyo ikiratibiwa kutajwa hapo kesho ambako mwelekeo kuhusu ombi la dhamana […]

KIVUMBI UCL: REAL MADRID v BAYERN, SPORTING v ARSENAL

Ligi kuu ya Mabingwa barani Ulaya inarejea kwa kishindo huku mechi mbili zikichezwa usiku wa Leo. Real Madrid watakua uwanjani Santiago Bernebeau kupambana na mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich katika mchezo wa kukata na shoka unaosubiriwa na mashabiki Wengi duniani. Bayern hawana rekodi nzuri dhidi ya Madrid na hivyo watakua wakiangazia kuiweka rekodi hiyo nyuma. […]