KIPKORIR ALENGA KUVUNJA REKODI YA SEKUNDE 43

Mshindi wa medali ya fedha ya Mashindano ya Afrika 2024, Kelvin Kipkorir, amesema analenga kushusha muda wake wa mita 400 hadi sekunde 43 mapema mwaka huu anapolenga kujumuishwa katika kikosi cha Kenya cha World Relays. Mwanariadha huyo wa Kenya Prisons kwa sasa ana rekodi binafsi ya sekunde 44.80, aliyoiweka katika Mashindano ya Kitaifa mwaka jana […]

ELIUD KIPCHOGE ACHAGULIWA KUBEBA BENDERA YA OLIMPIKI

Shujaa wa marathon wa Kenya, Eliud Kipchoge, ameteuliwa kuwa mmoja wa wabeba bendera rasmi wa Olimpiki katika Michezo ya Barafu ya Milano Cortina 2026. Kipchoge atashika bendera ya Olimpiki wakati wa sherehe za ufunguzi kwenye Uwanja wa San Siro, Milan, Ijumaa hii Uteuzi wake na Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa umemweka miongoni mwa watu wanane […]

OTUOMA AFIKA EACC KUHUSIANA NA UCHUNGUZI BUSIA

Gavana wa Busia Paul Otuoma amefika mbele ya Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) kufuatia wito kuhusu uchunguzi unaoendelea katika serikali ya Kaunti ya Busia. Otuoma alifika katika afisi za EACC Kanda ya Magharibi, Bungoma, ambapo ametakiwa kutoa taarifa kwa wachunguzi kufuatia madai ya ufisadi katika kaunti hiyo. Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

MCAs WA KIAMBU WADAI KUTISHIWA

Baadhi ya Wabunge wa Kaunti ya Kiambu wanaomuunga mkono Gavana Kimani Wamatangi wamedai kuwa wanapitia vitisho na hofu kabla ya kufunguliwa tena kwa Bunge la Kaunti wiki ijayo. Wabunge hao wanasema kuna mpango ulioratibiwa wa kubadilisha uongozi wa Bunge hilo, ukiwemo kuondolewa kwa Spika Charles Thiongo. Kulingana nao, hatua hiyo inalenga kufungua njia ya hoja […]

MAHAKAMA YAKATAA KUSITISHA UTEUZI WA WASHAURI WA RAIS

Mahakama Kuu imetupilia mbali maombi yaliyokuwa yakitaka kusimamisha uteuzi wa washauri wa rais, ikisema suala hilo tayari liliamuliwa awali. Jaji Bahati Mwamuye amesema wahusika waliorejea mahakamani waliwasilisha hoja zilezile na kuomba afueni sawa na zilizokuwa zimejadiliwa na kuamuliwa. Jaji huyo amebainisha kuwa hoja zilizotolewa wakati wa kusikilizwa kwa maombi hayo zilikuwa marudio tu, akisisitiza kuwa […]

MBADI APUUZA SIASA, AELEKEZA MACHO MAENDELEO

Waziri wa Fedha John Mbadi amepuuzilia mbali mjadala kuhusu mustakabali wake wa kisiasa huku taifa likielekea uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, akisema hilo si jambo linalomsumbua kwa sasa. Mbadi amsema kipaumbele chake ni kujenga Kenya yenye maendeleo na kuhakikisha sera za kiuchumi zinawanufaisha wananchi, badala ya kujihusisha na siasa za kujilinda kazini baada ya uchaguzi. […]

MGOMO WA WAFANYIKAZI WA SUKARI WASITISHWA

Mgomo wa nchi nzima wa wafanyikazi wa viwanda vya sukari umesitishwa kufuatia mazungumzo kati ya Serikali na Muungano wa Vyama vya Kupanda Sukari na Wafanyakazi Washirika nchini (KUSPAW). Ukiongozwa na waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe, mkutano uliofanyika katika jumba la Kilimo umeidhinisha kutolewa kwa shilingi bilioni 1 katika muda wa wiki mbili zijazo ili kupunguza matatizo ya mara moja […]

CHELSEA, ARSENAL KUTOA KIJASHO LEAGUE CUP

Kocha mkuu wa klabu ya Chelsea Liam Rosenior amekiri kuwa kujumuishwa kikosini kwa Estevao Willian dhidi ya Arsenal leo usiku kwenye mkondo wa mwisho wa semi fainali na taji la Carabao bado ni wa kutiliwa shaka. Raia huyo wa Brazil alikosa mechi dhidi ya West ham wikendi alipokuwa amerejea nyumbani kwao kwa likizo ya kibinafsi. […]

POLICE FC WATELEZA ZAIDI

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka nchini, KPL, Police FC wamejipata alama 11 nyuma ya viongozi wa ligi hiyo baada ya kushikwa katika sare ya bao 1-1 nyumbani dhidi ya Bidco United wanaokabiliwa na hatari ya kushushwa daraja. Mabao yote mawili yalifungwa katika dakika 10 za majeruhi, kwanza, Victor Kunyili akitishia kuwakaanga maafande kwa […]

UBADHIRIFU WA FEDHA BUNGOMA

Tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC inatarajiwa kuanzisha uchunguzi katika Sakata ya ufujaji wa shilingi milioni 3.6 katika kaunti ya Bungoma, zinazoripotiwa kuwasha taa ya mti wa Krisimasi mnamo mwaka wa 2019. Haya yamebainika gavana wa Bungoma Ken Lusaka alipofika mbele ya kamati ya uhasibu katika bunge la seneti, huku akikabiliwa na maswali kuhusu […]