OTUOMA AFIKA EACC KUHUSIANA NA UCHUNGUZI BUSIA

Gavana wa Busia Paul Otuoma amefika mbele ya Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) kufuatia wito kuhusu uchunguzi unaoendelea katika serikali ya Kaunti ya Busia. Otuoma alifika katika afisi za EACC Kanda ya Magharibi, Bungoma, ambapo ametakiwa kutoa taarifa kwa wachunguzi kufuatia madai ya ufisadi katika kaunti hiyo. Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

MCAs WA KIAMBU WADAI KUTISHIWA

Baadhi ya Wabunge wa Kaunti ya Kiambu wanaomuunga mkono Gavana Kimani Wamatangi wamedai kuwa wanapitia vitisho na hofu kabla ya kufunguliwa tena kwa Bunge la Kaunti wiki ijayo. Wabunge hao wanasema kuna mpango ulioratibiwa wa kubadilisha uongozi wa Bunge hilo, ukiwemo kuondolewa kwa Spika Charles Thiongo. Kulingana nao, hatua hiyo inalenga kufungua njia ya hoja […]

MAHAKAMA YAKATAA KUSITISHA UTEUZI WA WASHAURI WA RAIS

Mahakama Kuu imetupilia mbali maombi yaliyokuwa yakitaka kusimamisha uteuzi wa washauri wa rais, ikisema suala hilo tayari liliamuliwa awali. Jaji Bahati Mwamuye amesema wahusika waliorejea mahakamani waliwasilisha hoja zilezile na kuomba afueni sawa na zilizokuwa zimejadiliwa na kuamuliwa. Jaji huyo amebainisha kuwa hoja zilizotolewa wakati wa kusikilizwa kwa maombi hayo zilikuwa marudio tu, akisisitiza kuwa […]

MBADI APUUZA SIASA, AELEKEZA MACHO MAENDELEO

Waziri wa Fedha John Mbadi amepuuzilia mbali mjadala kuhusu mustakabali wake wa kisiasa huku taifa likielekea uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, akisema hilo si jambo linalomsumbua kwa sasa. Mbadi amsema kipaumbele chake ni kujenga Kenya yenye maendeleo na kuhakikisha sera za kiuchumi zinawanufaisha wananchi, badala ya kujihusisha na siasa za kujilinda kazini baada ya uchaguzi. […]

MGOMO WA WAFANYIKAZI WA SUKARI WASITISHWA

Mgomo wa nchi nzima wa wafanyikazi wa viwanda vya sukari umesitishwa kufuatia mazungumzo kati ya Serikali na Muungano wa Vyama vya Kupanda Sukari na Wafanyakazi Washirika nchini (KUSPAW). Ukiongozwa na waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe, mkutano uliofanyika katika jumba la Kilimo umeidhinisha kutolewa kwa shilingi bilioni 1 katika muda wa wiki mbili zijazo ili kupunguza matatizo ya mara moja […]

CHELSEA, ARSENAL KUTOA KIJASHO LEAGUE CUP

Kocha mkuu wa klabu ya Chelsea Liam Rosenior amekiri kuwa kujumuishwa kikosini kwa Estevao Willian dhidi ya Arsenal leo usiku kwenye mkondo wa mwisho wa semi fainali na taji la Carabao bado ni wa kutiliwa shaka. Raia huyo wa Brazil alikosa mechi dhidi ya West ham wikendi alipokuwa amerejea nyumbani kwao kwa likizo ya kibinafsi. […]

POLICE FC WATELEZA ZAIDI

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka nchini, KPL, Police FC wamejipata alama 11 nyuma ya viongozi wa ligi hiyo baada ya kushikwa katika sare ya bao 1-1 nyumbani dhidi ya Bidco United wanaokabiliwa na hatari ya kushushwa daraja. Mabao yote mawili yalifungwa katika dakika 10 za majeruhi, kwanza, Victor Kunyili akitishia kuwakaanga maafande kwa […]

UBADHIRIFU WA FEDHA BUNGOMA

Tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC inatarajiwa kuanzisha uchunguzi katika Sakata ya ufujaji wa shilingi milioni 3.6 katika kaunti ya Bungoma, zinazoripotiwa kuwasha taa ya mti wa Krisimasi mnamo mwaka wa 2019. Haya yamebainika gavana wa Bungoma Ken Lusaka alipofika mbele ya kamati ya uhasibu katika bunge la seneti, huku akikabiliwa na maswali kuhusu […]

WAFANYAKAZI KUPATA AFUENI YA PAYE

Huenda wakenya wanaopata mshahara wa chini ya shilingi 30,000 kwa mwezi wakapata afueni kutokana na mpango wa serikali kuwaondolea mzigo wa ushuru wa mapato maarufu kama Pay As You Earn, PAYE. Akizungumza katika mkutano wa kukusanya maoni ya wakenya, Waziri wa fedha John Mbadi amesema mpango huo pia utawalenga wanaopata chini ya shilingi 50,000 ambao […]

MGOMO WA MAAFISA WA KLINIKI WATAMATIKA

Hatimaye maafisa wa kliniki wametia saini mkataba wa Pamoja na serikali za kaunti, katika juhudi za kutamatisha vuta nikuvute ya muda mrefu ambayo imekuwa ikitatiza utoaji huduma za matibabu kwa wakenya. Kwenye mkataba huo uliotiwa saini kati ya muungano wa maafisa hao KUCO na serikali zote za kaunti 47, maafisa hao watapata nyongeza ya mshahara […]