EPL: MAN UNITED KUVAANA NA WESTHAM

Ligi kuu ya uingereze inaendelea usiku wa leo mechi kadhaa zikiratibiwa kuchezwa. Mwendo wa saa nne unusu usiku kutakuwa na mechi tatu ambapo Tottenham Hotspur watakuwa wanaazimia kuweka masaibu ya wikendi kando watakapowaalika Newcastle huku kukiwa na presha kubwa kwa makocha wa timu hizo mbili. Mechi nyingine itakua kati ya Chelsea na Leeds katika uwanja […]

KCB BANK KUFADHILI SAFARI RALLY KENYA 2026

Benki ya KCB Kenya imetenga KSh227 milioni kwa ajili ya World Rally Championship (WRC) Safari Rally Kenya 2026, ikish marking ufadhili wa mwaka wa sita mfululizo tangu rally hiyo maarufu irudi nchini baada ya miaka 19. Kati ya kiasi hiki, KSh100 milioni itapelekwa moja kwa moja kwa Safari Rally Kenya, huku KSh28.5 milioni zikitumika kwa […]

HSBC SEVENS YAPATA UFADHILI ZAIDI

Shindano la HSBC Sevens, linalotarajiwa kufanyika wiki hii katika Uwanja wa Taifa wa Nyayo, limepata msaada mkubwa baada ya kampuni ya mawasiliano Safaricom, kupitia chapa yake ya M-PESA, kutoa KSh10 milioni kwa ajili ya hafla hiyo. Victor Odada, Kiongozi wa Ushirikiano na Mipango  wa M-PESA, amesisitiza umuhimu wa kushiriki kwa wakenya wote katika mashindano haya, akiwataka mashabiki kuja […]

RIPOTI: SHERYL ADHIAMBO ALIFARIKI KWA JERAHA LA RISASI

Uchunguzi wa maiti umebaini kuwa Sheryl Adhiambo, mwanafunzi wa miaka 21 wa Chuo cha Mafunzo ya Madaktari cha Kenya (KMTC), alifariki dunia kutokana na jeraha moja la risasi kichwani. Uchunguzi huo, uliofanywa na wanapatholojia Grace Midigo na Simon Omuok, uligundua kuwa risasi iliingia upande wa kushoto wa kichwa chake na kutoka nyuma, na kusababisha kupasuka kwa […]

VIONGOZI WA TAITA TAVETA WALAANI UKEKETAJI

Viongozi kutoka kaunti ya Taita Taveta wanasema kuna haja ya juhudi zaidi hapa nchini ili kumaliza ukeketaji. Wakizungumza katika kaunti hiyo viongozi hao Wamesema visa vya ukeketaji vimekuwa vikiendelezwa hasa katika maeneo ya mipakani mwa Kenya na Tanzania. Aidha, viongozi hao wamesema ukeketaji unafanywa sio tu kwa wasichana wa shule za msingi na upili, bali pia […]

WAKILI AISHTAKI BUNGE KUHUSU FEDHA

Wakili mmoja wa Nairobi, Lempaa Suyianka, amewasilisha ombi kikatiba katika Mahakama Kuu akitaka Bunge na taasisi husika kufichua kiasi cha fedha za umma kilichotumika kuandaa hafla ya National Prayer Breakfast ya mwaka 2025. Katika ombi hilo, Lempaa ameshtaki Tume ya Huduma za Bunge, Bunge la Kitaifa, Seneti, Mwanasheria Mkuu na Tume ya Haki ya Utawala, […]

SENETI YAKANUSHA JARIBIO LA COG KUSITISHA UKAGUZI

Seneti imekanusha jaribio la baraza la Magavan la kusitisha kufika mbele ya kamati zake za ukaguzi wa kaunti. Seneti imesema hatua kama hizo zinaharibu uwajibikaji na ugatuzi. Spika Amason Kingi amesema Seneti inashughulikia kwa “wasiwasi mkubwa” madai ya magavana kuwa wanakabiliwa na vitisho, uonevu na rushwa kutoka kwa wanakamati. Baraza la Magavana pia lilitaka kuundwa upya kwa Kamati ya Hesabu za […]

GACHAGUA ATAKA SERIKALI KUTANGAZA UKAME JANGA LA KITAIFA.

Kinara wa DCP Rigathi Gachagua sasa anataka serikali itangaze hali ya ukame nchini kuwa janga la kitaifa. Akizungumza na wanahabari, Gachagua amesema eneo la kaskazini mwa Kenya lililoathirika zaidi linahitaji msaada wa dharura. Gachagua Pia amewalaumu viongozi wa kaskazini mashariki kwa kusalia kimya, licha ya ukame kumaliza mifugo na kuathiri wakaazi wake. Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

MAN CITY WALENGA KUPUNGUZA MWANYA DHIDI YA ARSENAL

Manchester City wana fursa ya kupunguza mwanya wa pointi kati yao na viongozi wa ligi ya EPL Arsenal hadi pointi 3 hapo kesho watakapoialika Fulham kabla ya Arsenal kufunga safari kucheza na Brentford walio katika fomu nzuri baadaye Alhamisi. The Gunners wanasalia katika nafasi nzuri ya kunyakua taji la EPL baad aya kusubiri kwa zaidi […]

RONALDO ATAMATISHA MGOMO WAKE

Nyota wa soka Cristiano Ronaldo ameripotiwa kutamatisha mgomo wake dhidi ya klabu yake ya Al-Nassr inayoshiriki ligi kuu ya Saudi Pro nchini Saudi Arabia, baada ya klabu hiyo kukubali matakwa yake kadhaa. Mchezaji huyo mahiri amekosa mechi 2 mfululizo licha ya mshahara mnono wa Euro 448,000 kwa wiki, ambazo ni takribani shilingi milioni 78.8 za […]