WAZOA TAKA DANDORA WASHINDA KESI

Mahakama ya Mazingira na Ardhi ya Milimani imeamuru kulipwa fidia ya shilingi milioni 25.8 kwa wazoa taka 1,032 wanaofanya kazi katika dampo la Dandora, baada ya kubaini kuwa haki zao za kikatiba zilikiukwa kutokana na kuathiriwa kwa muda mrefu na uchafuzi wa hewa. Katika uamuzi wake, Jaji Anne Omollo ameamua kwa niaba ya wazoa taka hao dhidi ya Serikali […]

SERIKALI KUIMARISHA UTAFITI NA UBUNIFU VYUONI

Rais William Ruto amesema Serikali inaweka utafiti na ubunifu kuwa nguzo kuu katika mafunzo ya elimu ya juu ili kukuza maarifa na ushindani wa taifa. Ruto amesema kuanzishwa kwa idara maalum ya serikali ya sayansi, utafiti na ubunifu kunadhihirisha dhamira ya kitaifa ya kuimarisha mafunzo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati, (STEM). Aidha Ruto Amesisitiza kuwa hatua hiyo […]

IEBC YAMTEUA SUNKULI KUWA KAIMU CEO

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC, imemteua Moses Ledama Sunkuli kuwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu na Katibu wa Tume. IEBC imesema kuwa Sunkuli, ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Operesheni za Uchaguzi, atahudumu kwa nafasi ya kaimu kwa kipindi cha miezi sita au hadi mchakato wa kuajiri afisa mkuu mtendaji wa kudumu utakapokamilika. Nafasi hiyo iliachwa wazi baada […]

TIMBER: ARSENAL WANA ARI YA UBINGWA

Mlinzi wa Arsenal, Jurrien Timber, anaamini kuinua Kombe la Ligi ya Uingereza kunaweza kuhamasisha Gunners kufanikisha mafanikio zaidi msimu huu. Timu ya Mikel Arteta ipo dakika 90 kutoka kumalizia miaka sita bila taji kuu baada ya kuiondoa Chelsea kwenye uwanja wa Emirates Jumanne, na kuhakikisha nafasi katika fainali itakayofanyika mwezi ujao. Arsenal pia wanaongoza ligi […]

KAYCI ODHIAMBO :AFC LEOPARDS TAYARI KWA UBINGWA

Mlinzi wa kati wa AFC Leopards, Kayci Odhiambo, amesema klabu ina imani na msukumo unaohitajika kumalizia kipindi cha miaka 28 bila taji lolote. Odhiambo, ambaye amekuwa mchezaji muhimu wa Leopards katika wiki za hivi karibuni, anasema hisia mpya ya umoja na malengo ndani ya kikosi inaweza hatimaye kuwaletea mashabiki wa klabu hiyo wenye subira matokeo […]

KAKAMEGA HOMEBOYZ YAOMBOLEZA MLINZI SILAS ABUNGANA

Kakamega Homeboyz FC na familia ya soka nchini Kenya wamegubikwa na mshtuko kufuatia kifo cha ghafla cha mlinzi wao, Silas Abungana. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, aliyekuwa amejiunga na klabu hiyo kutoka Shabana mwanzoni mwa msimu huu, alidaiwa kushambuliwa na ndugu yake mdogo katika mzozo mkali kuhusu kipande cha ardhi ya familia. Mchezaji […]

KENYA POLICE BULLETS WASHIKILIA TANGAZO LA UBINGWA

Wakilinda ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake FKF, Kenya Police Bullets, wameweka wazi nia yao ya kulinda taji lao baada ya kukamilisha usajili wa mshambuliaji nyota, Tereza Engesha. Kocha mkuu David Vijago anasema kuwa kuwasili kwa mchezaji huyo stadi anayehesabiwa kama moja ya usajili mkubwa katika historia ya hivi karibuni ya ligi, kutaondoa hofu ya kufunga magoli na […]

KENYA YAFUZU MASHINDANO YA VIKAPU 3X3

Kenya imefanikiwa rasmi kufuzu kushiriki mashindano ya mpira wa kikapu ya wachezaji watatu kwa timu za wanaume na wanawake katika Michezo ya Commonwealth itakayofanyika kuanzia Julai 24 hadi 29 katika ukumbi wa SEC, Jijini Glasgow Scotland. Waandalizi wa michezo hiyo wamethibitisha orodha ya mataifa yatakayoshiriki katika mchezo huo unaokua kwa kasi, ambao ulianza kushirikishwa rasmi katika Michezo ya […]

KENYA, UCHINA KUTIA SAINI MKATABA WA KUFIKIA BILA USHURU 

Serikali kuu inatazamiwa kutia saini mkataba wa kibiashara wa bidhaa bila Ushuru, Bila Upendeleo (DFQF) na Uchina ndani ya siku 30 zijazo, hatua inayotarajiwa kukuza mauzo ya nje ya kilimo nchini humo na kusawazisha uhusiano wake wa kibiashara wa muda mrefu na uchumi wa pili kwa ukubwa duniani. Katika mahojiano kwenye kituo kimoja cha runinga, Waziri wa Uwekezaji, […]

RISASI KWA WAANDAMANAJI: MBUNGE AOMBA MSAMAHA

Mbunge wa Belgut Nelson Koech hatimaye ameomba msamaha kuhusiana na matamshi yake ya kutaka polisi watumie risasi na kuwaua waandamanaji wanaozua vurugu yapata miezi 8 iliyopita. Kwenye mazungumzo na kituo kimoja cha runinga mapema leo, Koech ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusu ulinzi, ujasusi na masuala ya kigeni, amesikitikia kauli hizo, anazosema […]