SERIKALI YAKEMEA VURUGU ZA KISIASA

Serikali imekemea vikali vurugu za kisiasa na machafuko yanayoshuhudiwa ikisema yanahatarisha usalama wa wananchi na utulivu wa nchi Msemaji wa serikali Isaac Mwaura amesema makundi ya kihalifu yamekuwa yakijipenyeza katika maandamano huku akisisitiza kuwa maandamano ya amani yanalindwa kisheria Serikali imeonya dhidi ya uhamasishaji wa makundi yenye silaha na kusisitiza kuwa wafadhili wa vurugu watachukuliwa […]

WATU KADHAA WAKAMATWA KATIKA MAANDAMANO YA MAFUTA NAIROBI

Takriban watu kumi na mmoja wamekamatwa baada ya kujaribu kuandamana jijini Nairobi kupinga kupanda kwa bei ya mafuta Polisi wa kutuliza ghasia waliwatawanya waandamanaji hao walipokuwa wakijaribu kuelekea katikati ya jiji kutoka eneo la Archives na kuwapeleka katika kituo cha polisi cha Central Kamanda wa polisi wa Nairobi Issa Mohamud amesema maafisa walikuwa wakishirikiana na […]

WOLVES WAIAGA EPL NA NYUNDO YA WEST HAM

Klabu ya Wolves imekuwa ya kwanza kushushwa daraja kutoka ligi kuu ya soka nchini Uingereza, EPL, msimu huu, wakiratibiwa kushiriki ligi ya Championship msimu ujao. Wolves walio katika nafasi ya mwisho kwenye jedwali la EPL, walipokezwa kichapo cha mabao 3-0 na Leeds Jumamosi, na sare ya kutofungana kati ya West Ham na Crystal Palace jana […]

LOKEDI, KORIR WATETEA MATAJI YAO BOSTON

Mabingwa watetezi katika mbio za Boston Marathon Sharon Lokedi na John Korir waliiletea Kenya fahari kwa kutetea mataji yao katika mbio hizo hapo jana, wawili hao wakionyesha weledi na kuandikisha ubingwa mfululizo katika makala hayo ya 130. Ubingwa wa Korir ulikuwa wake wa 4 katika mbio za marathon, akianza kwa kasi na kuwapiku wenzake katika […]

KCB, KPC KUMENYANA SEMI FAINALI YA CAVB

Mabingwa wa zamani KCB walitinga awamu ya semi fainali ya mashindano ya ubingwa wa klabu za voliboli za wanawake barani Afrika jijini Cairo, Misri, kufuatia ushindi wao mnono wa seti za moja kwa moja dhidi ya Mayo Kanp Evolution ya Cameroon kwenye robo fainali za hapo jana. Wanabenki hao walionyesha mchezo wa aina yake kupata […]

WAATHIRIWA WA MAANDAMANO WATHIBITISHWA

Jumla ya waathiriwa 1,800 wamethibitishwa kuathirika na ukiukaji wa haki za kibinadamu wakati wa maandamano, orodha ya waathiriwa hao ikiratibiwa kuwasilishwa kwa Rais William Ruto kabla ya mchakato wa fidia kuanza. Tume ya kitaifa kuhusu haki za kibinadamu, KNCHR, imethibitisha malalamishi ya waathiriwa hao, na kupendekeza fidia ya shilingi milioni 3 kwa waliouawa na shilingi […]

UHABA WA MBOLEA WAZUA HOFU

Serikali imetakiwa kuchukua hatua za haraka na kuhakikisha upatikanaji wa mbolea ya kunyunyiza mazao ili kuepusha hatari ya kuathirika kwa mavuno na kusambaratisha juhudi za kuimarisha uteshelezi wa chakula. Wakulima katika maeneo mbali mbali nchini hasa katika kaunti ya Trans Nzoia, wamelalamikia uhaba wa mbolea hiyo katika maghala ya bodi ya nafaka, wakihofia kuathirika kwa […]

RUTO AKEJELI MAANDAMANO KUHUSU MAFUTA

Rais William Ruto ameendelea kutetea hatua ya Kenya kuuza mafuta kwa bei ya juu ikilinganishwa na mataifa jirani, huku akiwakejeli wanaopanga maandamano ya kushinikiza kupunguzwa kwa bei hiyo akisema hatua yao haitatoa suluhu. Akizungumza na wakenya wanaoishi nchini Italia anakofanya ziara, Ruto amewakosoa waandalizi wa maandamano hayo akisema wanalenga kuwapotosha wakenya. Amekariri kuwa ada za […]

SIKU YA MAANDAMANO HII HAPA

Maandamano yameratibiwa kufanyika katika maeneo mbali mbali ya nchi hii leo ambapo waandalizi wanalalamikia bei ya juu ya mafuta iliyotangazwa wiki jana na serikali. Kupitia kauli mbiu ya Reject Fuel Prices, wakenya wanalenga kuishinikiza serikali kupunguza bei ya mafuta mbali na kuangazia gharama ya juu ya maisha ambayo imechangiwa na ongezeko la bei hizo. Jijini […]

GACHAGUA: WAFUASI WETU WANANYIMWA VITAMBULISHO

Huku vijana wakikosolewa kutokana na idadi ndogo ya wanaojitokeza kusajiliwa kama wapiga kura, aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua ameibua madai kwamba serikali inachelewesha maksudi utoaji wa vitambulisho vya kitaifa kwa vijana walio katika maeneo yanayodhaniwa kuwa ngome za upinzani. Gachagua ameshikilia kuwa hatua hiyo inasambaratisha zoezi la usajili wa wapiga kura wapya, akitishia kuwaongoza vijana […]