POLISI WAKAMATA WAHUNI ZAIDI YA 80 NAIROBI

Takriban wahuni themanini na wanne wamekamatwa katika oparesheni za polisi zilizotekelezwa katika wiki za hivi karibuni jijini Nairobi huku juhudi za kudhibiti uhalifu zikiongezwa Kamanda wa polisi kanda ya Nairobi Issa Mohamud amesema wameimarisha doria zinazoongozwa na taarifa za kiintelijensia ili kukabiliana na vitendo vya uhalifu vinavyoendelea jijini Ameonya kuwa hawatavumilia matumizi ya wahuni kutisha […]

DUALE AONYA HOSPITALI KUHUSU ULAGHAI WA SHA

Waziri wa Afya Aden Duale ameonya vituo vya afya vinavyoshiriki katika mpango wa mamlaka ya afya ya jamii akisema vitakavyohusika na vitendo vya ulaghai vitafutiwa mikataba mara moja Akizungumza katika hospitali ya rufaa ya kaunti ya Bungoma Duale amesema mageuzi ya kidijitali yanayoendelea yanalenga kuimarisha uwazi uwajibikaji na utoaji wa huduma bora huku akiwataka wasimamizi […]

POLISI NAIROBI WAKATAA MAANDAMANO YALIYOPANGWA

Kamanda wa polisi jijini Nairobi Issa Mohamud amesema maandamano yaliyopangwa kufanyika Jumanne Aprili ishirini na moja hayatambuliwi kisheria kwa kuwa Hakuna taarifa rasmi iliyowasilishwa kwa Huduma ya Polisi nchini Kauli hiyo inajiri kufuatia malalamishi ya Wakenya mtandaoni kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta ambapo baadhi yao walikuwa wameitisha maandamano kupitia jumbe zilizosambaa katika mitandao ya kijamii […]

WANAFUNZI WA UON WAPINGA MAANDAMANO YA UPINZANI.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nairobi wamepinga hoja ya maandamano ya viongozi wa upinzani kulalamikia bei ya mafuta. Wanfunzi hao wamesema kuwa bei ya mafuta haijaathiriwa humu nchini pekee bali pia ni mfumuko ambao umeathiri dunia kiujumla Aidha wamewataka viongozi kutotumia kupanda kwa bei ya mafuta kujinufaisha kisiasa huku wakisema maandamano sio suluhisho. Imetayarishwa na […]

CITY YATHIBITISHA SILVA KUONDOKA ETIHAD

Klabu ya Manchester City imetangaza kwamba nahodha wake Bernardo Silva ataondoka mwishoni mwa msimu huu kandarasi yake itakapokamilika. Silva mwenye umri wa miaka 31, alijiunga na City kwa kima cha pauni milioni 43 mwaka 2017 akitokea klabu ya Monaco nchini Ufaransa, na ameichezea klabu hiyo zaidi ya mechi 450 chini ya meneja Pep Guardiola na […]

VILLA WAITANDAZA BOLOGNA KUWEKA MIADI NA FOREST

Klabu ya Aston Villa ilijikatia tiketi ya nusu fainali ya michuano ya UEFA UROPA League ambako watamenya na Nottingham Forest katika pambano litakalokutanisha klabu hizo za EPL baadaye mwezi huu. Hii ni kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Bologna jana usiku na kufikisha ushindi wa jumla ya mabao 7-1 kutokana na ushindi wa mabao […]

JUNIOR STARLETS WAREJEA

Timu ya taifa ya soka ya wanawake chipukizi Junior Starlets imerejea nchini kutoka Namibia ambako waliilaza wenyeji mabao 2-1 katika mashindano ya kuwania tiketi ya kufuzu mashindano ya FIFA U17 Women. Kwa sasa chipukizi hao wanajiandaa kwa mechi ya marudiano dhidi ya wageni wao wikendi hii, na wameelekea moja kwa moja kwenye kambi ya mazoezi. […]

BEI YA MAFUTA: RUTO ATAKIWA KUPANDISHA MISHAHARA

Rais William Ruto ametakiwa kupandisha kiwango cha chini cha mishahara ya wafanyakazi wa ngazi ya chini kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha. Katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyakazi, COTU, Francis Atwoli, amesema kuwa ongezeko la bei ya mafuta litapandisha gharama hiyo moja kwa moja. Ametaka hatua hiyo kutangazwa rasmi kabla ya maadhimisho […]

KENHA YAONYA USAFIRI UTASAMBARATIKA MAI MAHIU-SUSWA

Madereva wanaotumia barabara ya Mai Mahiu kuelekea Suswa hadi Narok wameonywa kuhusu kusambaratika kwa shughuli za usafiri kwenye barabara hiyo kutokana na mafuriko yaliyokusanya matope katika maeneo kadhaa ya barabara hiyo. Kulingana na mamlaka ya barabara kuu nchini, KeNHA, maeneo yaliyoathirika ni Kedong Ranch, ambako hali ya barabara imedorora kutokana na mvua kubwa. KeNHA imesema […]

MUKHISA AAGIZWA NA CUE KUHUSU MADAI DHIDI CHUO

Tume inayosimamia elimu ya vyuo vikuu, CUE, imemwagiza aliyekuwa katibu mkuu wa idara ya biashara na ustawi chini ya Umoja wa Mataifa, Mukhisa Kituyi, kufika mbele yake kuhusiana na kauli alizotoa kuhusu chuo kikuu cha Masinde Muliro. Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, CUE imesema Mukhisa, akiwa kwenye mahojiano na kituo cha redio tarehe 31 […]