UHABA WA MAFUTA WAVURUGA USAFIRI

Shughuli za uchukuzi zimeendelea kutatizika katika maeneo mbali mbali kutokana na uhaba wa mafuta ambao umesababisha kufungwa kwa vituo kadhaa vya kuuza mafuta. Kupitia taarifa, muungano wa wasafirishaji nchini umeonya kuwa huenda uhaba huo ukasambaratisha uchukuzi, huku wakenya wakiishinikiza serikali kuweka wazi hali halisi ya kiwango cha mafuta nchini. Serikali imeshikilia kuwa kuna akiba ya […]

SIFUNA ALIOMBA TENA JOPO KUMWOKOA

Katibu mkuu wa chama cha ODM na ambaye pia ni seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, amewasilisha tena ombi kwa jopo la kutatua migogoro ya kisiasa akitaka kufutiliwa mbali kwa uamuzi wa kamati kuu ya chama cha ODM kumtimua kutoka wadhifa wa katibu mkuu. Kupitia kwa mawakili wake, Sifuna ameorodhesha ombi hilo kama dharura, akitaka kusitishwa […]

KAGWE ATOA HAKIKISHO LA MBEGU

Wizara ya kilimo nchini imewataka wakulima kuondoa hofu kuhusiana mbegu, ikisema kuna akiba ya kutosha za upanzi msimu huu na mwaka mzima. Waziri wa kilimo Mutahi Kagwe, amesema kuwa serikali imeimarisha mikakati ya uzalishaji na usambazaji wa mbegu katika juhudi za kuhakikisha kila mkulima anafikiwa na mbegu kwa wakati. Amesema uwekezaji zaidi unaendelea katika sekta […]

RAIS WA CAF AFANYA ZIARA SENEGAL

Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Patrice Motsepe, amefanya ziara nchini Senegal takriban mwezi mmoja baada ya uamuzi wa kustaajabisha wa kuondoa Senegal kutoka ubingwa wa AFCON na kuutumia Morocco. Motsepe alitangaza safari hiyo mwishoni mwa Machi akisema atatembelea Senegal na Morocco ili kusisitiza umuhimu wa “kushirikiana kukuza soka barani Afrika,” huku shirikisho lake likikabiliwa […]

KENYA PIPELINE YALENGA UBINGWA AFRIKA

Kocha wa timu ya mpira wa wavu ya wanawake ya Kenya Pipeline, Geoffrey Omondi, amesema mashindano ya vilabu barani Afrika yatakayofanyika Misri ni kiwango cha chini wanacholenga kama mabingwa wa taifa. Omondi amesema timu hiyo ina kiu ya kutwaa ubingwa wa saba wa bara, sambamba na wawakilishi wengine wa Kenya wanaotarajia kufanya vyema katika mashindano […]

GOR MAHIA WATULIA KWENYE MBIO ZA UBINGWA

Mbio za ubingwa wa Ligi Kuu nchini zimepamba moto huku mabingwa watetezi Gor Mahia wakisalia watulivu licha ya presha kutoka kwa wapinzani wao wakuu AFC Leopards. AFC Leopards wamepunguza pengo la alama hadi mbili baada ya ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya Murang’a Seal, huku Gor Mahia wakiongoza jedwali kwa alama 57 na […]

KSSA: ST ANTONY’S YAIBUKA NA USHINDI KWENYE MAGONGO

Shule ya St Antony’s ya Kitale imeanza vyema mashindano ya kitaifa ya michezo ya shule za upili muhula wa kwanza baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya wenyeji Kisumu Day. Katika mchezo huo uliokuwa mkali, nyota wa timu hiyo Kevin Onyango alifunga bao pekee lililoipa ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya wapinzani wao. […]

UDA PWANI YAKATAA MPANGO WA KUTENGA MAENEO

Viongozi wa chama cha UDA kutoka ukanda wa pwani wamepinga hoja ya kutenga maeneo na nyadhifa katika uchaguzi mkuu ujao. Wakizungumza mjini Mombasa, viongozi hao wamesema watahakikisha vyama vyao na ODM vinashindana katika nyadhifa zote za pwani, wakipuuzilia mbali madai kuwa ODM kinaungwa mkono zaidi katika eneo hilo. Aidha, viongozi hao akiwemo Spika wa Seneti Amason […]

KUCCPS YAFUNGUA MAOMBI YA VYUO

Wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2025 pamoja na waliohitimu miaka ya awali sasa wanaweza kutuma maombi ya kujiunga na vyuo vikuu, vyuo vya kati na taasisi za mafunzo ya ufundi. Huduma ya upangaji wanafunzi vyuoni imetangaza kufunguliwa kwa dirisha la maombi ya mwaka 2026, ikiwahimiza wanafunzi kuchagua kozi na taasisi wanazopendelea. Dirisha […]

IEBC YAONGEZA MATAYARISHO YA UCHAGUZI

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC imeimarisha matayarisho ya Uchaguzi Mkuu wa 2027 kupitia kongamano la washikadau kuhusu usajili unaoendelea wa wapigakura lililofanyika Kiambu. Kongamano hilo limewaleta pamoja wadau mbalimbali kujadili mbinu bora za kuongeza idadi ya wapigakura wanaojiandikisha na kuboresha mchakato wa usajili nchini. Tume hiyo imesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wadau wote ili […]