BARASA ASUKUMA NAFASI YA ODM KAKAMEGA

Gavana wa Kakamega Fernandes Barasa ameendeleza kampeni za chama cha ODM katika kaunti hiyo akieleza sababu za Kakamega kupewa nafasi ya juu ya uongozi ndani ya chama hicho. Akizungumza Bukura, kaunti ndogo ya Lurambi, wakati wa ugawaji wa bidhaa za kilimo, Barasa alisema nafasi ya naibu kiongozi wa chama hicho inapaswa kutolewa kwa kiongozi kutoka […]

MAEGESHO HARAMU NAIROBI YAPINGWA

Mkaazi mmoja wa Nairobi amepinga kile anachodai kuwa maegesho haramu yanayofanywa na maafisa wa kaunti pamoja na wajumbe wa bunge la kaunti kwenye njia za waenda kwa miguu na maeneo ya watu wenye ulemavu katika barabara za jiji. Katika hoja zake, amesema hatua hiyo ni matumizi mabaya ya mamlaka na ukiukaji wa haki za wananchi, […]

UPINZANI WAMTAKA OMOLLO KUJIUZULU KISA SHAMBULIO LA OSOTSI

Viongozi wa upinzani wanamtaka katibu katika wizara ya usalama, Daktari Raymond Omollo, kujiuzulu kufuatia kushambuliwa kwa Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi katika hoteli moja jijini Kisumu. Viongozi hao Wanasema idara ya usalama inafahamu wahuni wanaohusika na mashambulizi dhidi ya wanaopinga serikali, na hivyo wanapaswa kuwajibika kwa hali hiyo. Kwa upande wake, Osotsi ameeleza yaliyotokea akisisitiza umuhimu […]

KENYA YAZINDUA MPANGO WA KUIMARISHA USIMAMIZI WA TABIANCHI WA KAMPUNI

Serikali kuu imezindua mpango wa “Chapter Zero” unaolenga kuimarisha usimamizi wa tabianchi katika sekta ya kampuni mbali mbali. Katibu Mkuu wa Wizara ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi Festus Ng’eno akizungumza katika uzinduzi huo mjini Nairobi, amesema kuwa mpango huo unaendeleza hatua za tabianchi na uendelevu wa mazingira. Ng’eno ameongeza kuwa serikali inakamilisha kanuni za ziada kuhusu […]

KPC YAZUNGUMZIA UHABA WA MAFUTA

Serikali kwa mara nyingine imetoa hakikisho kwamba kuna akiba za kutosha za mafuta nchini licha ya uhaba kuripotiwa katika baadhi ya maeneo na hata vituo kadhaa kufungwa kutokana na ukosefu wa mafuta. Kupitia taarifa, kampuni ya Kenya Pipeline, KPC, imesema akiba zake zote zina mafuta ya kutosha kama vile diseli, petroli na mafuta ya ndege […]

LIVERPOOL, BARCELONA WAPEPETWA ULAYA

Matumaini ya Liverpool kufuzu semi fainali ya dimba la klabu bingwa bara Ulaya yaliachwa njia panda baada ya kichapo cha kutamaushwa mikononi mwa mabingwa wa bara Ulaya PSG, kikiwa ni kichapo cha 16 msimu huu kwa vijana hao wa Arne Slot. Desire Doue aliiweka PSG kifua mbele kunako dakika ya 11 baada ya shuti lake […]

FKF CUP KUINGIA RAUNDI YA 16 IJUMAA

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka nchini KPL, Police FC, na washindani wa taji hilo Tusker FC watakuwa na kibarua kigumu katika raundi ya 16 ya kombe la FKF Cup hapo kesho katika uwanja wa Kasarani jijini Nairobi. Police FC watakabiliana na Daudi wa soka BB Bread waliowabandua AFC Leopards na Gor Mahia, nao […]

LUKENYA, KAMUSINGA ZAWIKA KWENYE VIKAPU

Shule za Lukenya na Friends School Kamusinga zilitawala mchezo wa vikapu katika mashindano ya kitaifa ya shule za upili kwa muhula wa kwanza yanayoendelea katika kaunti ya Kisumu. Shule hizo zilifuzu semi fainali za mashindano hayo kwa mchezo wa vikapu wa wachezaji 5 kila upande yaani 5×5, Lukenya wakiilaza Dagoretti 79-62 huku Kamusinga wakiibebesha Sabunley […]

WATTANGA ATEULIWA BAADA YA KRA

Aliyekuwa kamishna mkuu wa mamlaka ya kitaifa kuhusu ukusanyaji ushuru, KRA, Humphrey Wattanga, ameteuliwa kuwa balozi wa Kenya nchini Afrika Kusini, muda mfupi baada ya kuondoka KRA. Kulingana na mwenyekiti wa bodi ya mamlaka hiyo Ndiritu Muriithi, Wattanga alikuwa kwenye likizo ya mwisho kufuatia kukamilika kwa mkataba wake, kabla ya uteuzi wake na Rais William […]

DCI YACHUNGUZA UVAMIZI DHIDI YA OSOTSI

Idara ya upelelezi wa jinai DCI imeanzisha uchunguzi katika tukio la kutamausha ambapo seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi alishambuliwa na watu wasiojulikana katika jumba moja la kibiashara jijini Kisumu hapo jana. Kupitia taarifa, DCI imeshutumu tukio hilo, na kuongeza kuwa maafisa wake wameanzisha uchunguzi rasmi, na kwamba hadi sasa kiini cha uvamizi huo bado hakijabainika, […]