WAKENYA 16 WARIPOTIWA KUPOTEA URUSI

Waziri Mkuu wa Mawaziri na Waziri wa Mambo ya Nje, Musalia Mudavadi, amesema angalau Wakenya 16 wameripotiwa kupotea nchini Urusi. Mudavadi amesema idadi hiyo imeongezeka kutoka watu 10 hadi 16 ndani ya saa 24 zilizopita, huku hali halisi ya walipo bado haijabainika. Ameeleza kuwa suala hilo limezua wasiwasi mkubwa kitaifa, hasa kutokana na madai ya […]

MBADI: BEI YA MAFUTA IMEPANDA KIMATAIFA

Waziri wa Hazina ya Taifa, John Mbadi, amesema serikali itaingilia kati kuwalinda Wakenya dhidi ya kupanda kwa bei ya mafuta ya petroli katika soko la kimataifa. Mbadi amesema serikali itatumia fedha kutoka kodi ya maendeleo ya mafuta, inayokadiriwa kuwa shilingi bilioni 17, katika kipindi cha miezi mitatu ijayo ili kupunguza shinikizo la bei kwa watumiaji. […]

BUNGOMA HIGH YALENGA UBINGWA WA RAGA

Timu ya raga ya Bungoma High School inalenga kurejea historia ya mwaka 2016 kwa kutwaa ubingwa wa kitaifa wa raga ya wachezaji 15 katika michezo ya shule za upili itakayofanyika Kisumu Hii ni baada ya ushindi wao wa kanda ya magharibi walipowashinda Kakamega School alama 12-07 katika fainali iliyofanyika Chavakali High School mwezi uliopita. Kocha wao, Titus […]

TUCHEL: FODEN HANA UHAKIKA NA NAFASI YA KOMBE LA DUNIA

Kocha wa uingereza, Thomas Tuchel, amesema nafasi ya Phil Foden katika kikosi cha Kombe la Dunia haijahakikishwa, baada ya mchezaji huyo kushindwa kuonyesha kiwango cha juu tena katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Japan. Foden, mwenye umri wa miaka 25, alikumbana na changamoto kucheza katika nafasi isiyo ya kawaida mbele, huku Harry Kane akikosa kwenye mchezo huo. […]

ODUOR ALENGA NAFASI YA KUDUMU STARS

Kiungo wa ulinzi wa Harambee Stars, Clarke Oduor, analenga kujihakikishia nafasi ya kudumu katika kikosi hicho baada ya kuchangia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Grenada kwenye mashindano ya kimataifa jijini Kigali. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, anayekipiga kwa mkopo katika klabu ya Grimsby Town kutoka Bradford City, ameonyesha kiwango kizuri katika kurejea […]

SOFAPAKA YAKABILIWA NA HATARI YA KUSHUKA

Aliyekuwa kocha wa Harambee Stars, Twahir Muhiddin, amesema Sofapaka FC inahitaji “muujiza” ili kuepuka kushuka daraja katika Ligi Kuu ya FKF. Muhiddin ameeleza kuwa vita vya kushuka daraja bado viko wazi huku timu kadhaa zikiwa hatarini msimu ukikaribia tamati. Sofapaka iko mkiani mwa jedwali ikiwa na alama 15, alama 10 nyuma ya Kariobangi Sharks, ikiwa zimesalia mechi tisa pekee, […]

ST. ANTONY’S YALENGA UBINGWA KISUMU

Kocha wa timu ya magongo ya St. Antony’s Kitale, Kevin Lugalia, amesema kikosi chake kitachukulia kila mechi kama fainali katika michezo ya kitaifa ya shule za upili itakayoanza Jumatatu jijini Kisumu. Lugalia amesema timu imeimarisha maandalizi yake na inaamini ina uwezo wa kutwaa ubingwa katika mashindano hayo. St. Antony’s imepangwa katika Kundi A pamoja na […]

WAZIRI WA MICHEZO ITALIA AMTAKA MKUU WA SPOTI AONDOKE

Waziri wa michezo nchini Italia Andrea Abodi, amemtaka mkuu wa shirikisho la soka nchini humo kujiuzulu baada ya timu ya taifa ya soka ya taifa hilo, the Azzurri, kukosa kushiriki kombe la dunia kwa mara ya tatu mtawalia. Mabingwa hao wa dunia mara 4, walibanduliwa kupitia mechi ya mwondoano kwa mara nyingine tena baada ya […]

KISUMU TAYARI KWA MICHEZO YA KSSSA

Jumla ya washiriki 3,600 wameratibiwa kushiriki michezo ya kitaifa ya shule za upili kwa muhula wa kwanza, itakayong’oa nanga tarehe 6 na kukamilika tarehe 12 mwezi huu katika kaunti ya Kisumu. Kulingana na mkurugenzi wa masuala ya michezo katika wizara ya elimu Nelson Sifuna, ongezeko la idadi ya washiriki linaashiria matokeo ya mtaala wa umilisi […]

STARLETS WAJIANDAA KWA FIFA SERIES

Kikosi cha timu ya taifa ya kandanda ya wanawake Harambee Starlets imeanza kambi ya mazoezi, katika maandalizi ya michezo ya FIFA Series itakayoandaliwa hapa nchini. Miongoni mwa majina tajika katika kikosi cha awali cha wachezaji 31 kilichotajwa na kocha Beldine Odemba, ni Marion Serenge atakayechezea kikosi hicho kwa mara ya kwanza. Serenge alikuwa sehemu ya […]