ST. ANTONY’S YALENGA UBINGWA KISUMU

Kocha wa timu ya magongo ya St. Antony’s Kitale, Kevin Lugalia, amesema kikosi chake kitachukulia kila mechi kama fainali katika michezo ya kitaifa ya shule za upili itakayoanza Jumatatu jijini Kisumu. Lugalia amesema timu imeimarisha maandalizi yake na inaamini ina uwezo wa kutwaa ubingwa katika mashindano hayo. St. Antony’s imepangwa katika Kundi A pamoja na […]

WAZIRI WA MICHEZO ITALIA AMTAKA MKUU WA SPOTI AONDOKE

Waziri wa michezo nchini Italia Andrea Abodi, amemtaka mkuu wa shirikisho la soka nchini humo kujiuzulu baada ya timu ya taifa ya soka ya taifa hilo, the Azzurri, kukosa kushiriki kombe la dunia kwa mara ya tatu mtawalia. Mabingwa hao wa dunia mara 4, walibanduliwa kupitia mechi ya mwondoano kwa mara nyingine tena baada ya […]

KISUMU TAYARI KWA MICHEZO YA KSSSA

Jumla ya washiriki 3,600 wameratibiwa kushiriki michezo ya kitaifa ya shule za upili kwa muhula wa kwanza, itakayong’oa nanga tarehe 6 na kukamilika tarehe 12 mwezi huu katika kaunti ya Kisumu. Kulingana na mkurugenzi wa masuala ya michezo katika wizara ya elimu Nelson Sifuna, ongezeko la idadi ya washiriki linaashiria matokeo ya mtaala wa umilisi […]

STARLETS WAJIANDAA KWA FIFA SERIES

Kikosi cha timu ya taifa ya kandanda ya wanawake Harambee Starlets imeanza kambi ya mazoezi, katika maandalizi ya michezo ya FIFA Series itakayoandaliwa hapa nchini. Miongoni mwa majina tajika katika kikosi cha awali cha wachezaji 31 kilichotajwa na kocha Beldine Odemba, ni Marion Serenge atakayechezea kikosi hicho kwa mara ya kwanza. Serenge alikuwa sehemu ya […]

USAJILI WA MAKURUTU KUKUMBATIA AI

Mageuzi makubwa yanatarajiwa katika mfumo wa usajili wa makurutu wa kujiunga na idara ya polisi, serikali ikitangaza kutumia mfumo wa akiliunde, yaani Artificial Intelligence, AI, kuwasajili makurutu hao. Kulingana na Waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen, hatua hiyo inalenga kukiimarisha kikosi cha polisi kulingana na mageuzi ya kiteknolojia, akiongeza kuwa mfumo wa kidijitali utachukua […]

RUTO: REKODI YANGU ITANITETEA

Rais William Ruto amekariri kuwa rekodi yake ya maendeleo inatosha kumrejesha mamlakani kwa muhula wa pili kupitia uchaguzi mkuu ujao, akipuzilia mbali tetesi za upinzani kwamba serikali yake imefeli kutekeleza ahadi alizotoa kabla ya kuchaguliwa. Kulingana na Ruto, serikali yake iko katika mkondo mwafaka wa kutoa huduma kwa wananchi. Imetayarishwa na Antony Nyongesa

UHURU: MSICHEZE TENA NA MOTO!

Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta amewatahadharisha wakazi wa eneo la Mlima Kenya dhidi ya kumpigia kura Rais William Ruto, akiwaonya dhidi ya kurejelea alichokitaja kuwa makosa ya mwaka wa 2022. Uhuru aliyekuwa akizungumza katika hafla ya mazishi katika kaunti ya Kirinyaga, amewahimiza viongozi wa upinzani kuhakikisha umoja wa kitaifa. Naye aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua, akidokeza […]

GAVANA LELELIT ATISHIA KUWASHTAKI MASENETA

Mvutano kati ya maseneta na magavana kuhusu uwajibika wa magavana umechukua mkondo tofauti, gavana wa Samburu Lati Lelelit akitishia kuwashtaki maseneta wanaohudumu kwenye kamati ya uhasibu wa fedha za kaunti kwa madai ya kumdhalilisha katika majengo ya bunge hapo jana. Hii ni baada ya maseneta hao kujaribu kumkamata alipokuwa akiwahutubia wanahabari kwenye majengo hayo, siku […]

MAKUBALIANO YA KENYA-URUSI KUWAREJESHA WAKENYA NCHINI

Hatimaye serikali za Kenya na Urusi zimetia saini makubaliano yatakayowawezesha wakenya wanaolenga kujiondoa kwa hiari katika jeshi la Urusi na kurejea nchini kufanya hivyo Kulingana na mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi, zaidi ya wakenya 250 wanaaminika kujiunga na jeshi la Urusi kwenye mapigano dhidi ya Ukraine, akiweka wazi majina ya wakenya 2 wanaozuiliwa nchini Ukraine […]

TUCHEL AHOJI KIKOSI BAADA YA KIPIGO

Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Thomas Tuchel, amesema sasa ana uelewa zaidi kuhusu kikosi chake licha ya kipigo cha mabao 1-0 dhidi ya Japan katika mechi ya kirafiki. Tuchel alikuwa ameteua kikosi cha wachezaji 35 kwa mechi dhidi ya Uruguay na Japan, huku sare ya 1-1 dhidi ya Uruguay ikihusisha wachezaji wa akiba […]