WINNIE ODINGA AHUDHURIA KONGAMANO LA LINDA GROUND

Mbunge wa EALA ambaye pia ni Mwanawe Hayati Raila Odinga amejiunga na mkutano maalum wa Wajumbe wa chama cha ODM huko Jamhuri Grounds wiki chache baada ya kuidhinishwa kama mwakilishi wa Chama cha ODM. Hatua hiyo imejiri licha ya kuwepo kwa mkutano sambamba wa kundi la Linda Mwananchi katika Ukumbi wa Ufungamano, kundi ambalo amekuwa […]

KWS YAKANUSHA UHARIBIFU WA MSITU NAIROBI

Shirika la Huduma za Wanyamapori limekanusha madai yanayosambaa mitandaoni kwamba linaharibu msitu wa nyanda za juu katika Hifadhi ya Taifa ya Nairobi. Shirika hilo limesema madai hayo yanapotosha, likieleza kuwa kazi inayoendelea ni sehemu ya mpango halali wa kuhamisha kituo cha kulea wanyama yatima cha Nairobi. Aidha, limesema hatua hiyo inalenga kuboresha uhifadhi wa wanyamapori, […]

OBURU OGINGA AIDHINISHWA KIONGOZI WA ODM

Chama cha ODM kimemuidhinisha rasmi Seneta wa Siaya, Daktari Oburu Oginga, kuwa kiongozi wa chama hicho kufuatia kifo cha kaka yake na aliyekuwa kiongozi wa muda mrefu Raila Odinga. Daktari Oburu, aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo baada ya kupendekezwa na baraza la juu la chama, amepitishwa rasmi katika mkutano maalum wa wajumbe uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri. Katika […]

MSWADA WA FEDHA 2026 HAUNA USHURU MPYA, WAKENYA WAHAKIKISHIWA

Hazina ya Kitaifa imewahakikishia Wakenya na Bunge kwamba Mswada ujao wa Fedha wa 2026 hautaleta ushuru mpya au kuongeza viwango vya ushuru vilivyopo. Ahadi hiyo inalenga kupunguza wasiwasi wa umma na kukuza uthabiti wa kiuchumi kufuatia mizozo kuhusu ushuru katika miaka iliyopita. Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Hazina ya Kitaifa John Mbadi amefika mbele […]

FIFA WORLD CUP: ITALIA WAKARIBIA KUKATA KIU

Timu ya taifa ya kandanda ya Italia itachuana na Bosnia and Herzegovina kwenye fainali za mwondoano wa bara Ulaya kusaka tiketi ya kusakata dimba la kombe la dunia mwaka huu, baada ya kuandikisha ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Northern Ireland kwenye semi fainali za mchujo huo. Wakati uo huo, Wales na Jamhuri ya Ireland […]

UKAMILISHO WA TALANTA STADIUM WASUKUMWA MEI

Makataa ya kukamilishwa kwa ujenzi wa uwanja wa michezo wa Talanta Sports City imesongeshwa kutoka Machi hadi Mei, uwezekano mkubwa ukiwa kwamba huenda ujenzi huo ukakamilika Julai mwaka huu. Kuahirishwa huko kumejiri kufuatia ukaguzi wa kamati ya seneti kuhusu barabara, uchukuzi na miundombinu, inayosema imeridhishwa na hatua zilizopigwa hadi sasa. Aidha, lengo lao la ukaguzi […]

BINGWA WA ZAMANI WA U20 KUONJA BERLIN HALF MARATHON

Chipukizi wa Kenya Benson Kiplangat imeratibiwa kushiriki kwa mara ya kwanza mashindano ya half Marathon jijini Berlin Jumapili hii, ikiondokea mbio za masafa mafupi kuingia masafa marefu. Kinda huyo mwenye umri wa miaka 22, alitangaza uwepo wake katika fani ya riada katika mbio za ubingwa wa wanariadha wasiozidi umri wa miaka 20 mwaka wa 2021, […]

GACHAGUA AWAHIMIZA VIJANA KUJIHAMI NA KURA

Huku zoezi la kitaifa la kuwasajili wapiga kura wapya likiendelea, vijana kote nchini wamehimizwa kujitokeza na kusajiliwa kwa wingi ili kuafikia mabadiliko ya uongozi ambayo wamekuwa wakishinikiza kupitia maandamano. Kiongozi wa chama cha DCP Rigathi Gachagua, amesema muungano wa upinzani unategemea idadi kubwa ya wapiga kura wapya kumbandua madarakani Rais William Ruto kwenye uchaguzi mkuu […]

UPASUAJI WA MAITI KUENDELEA KERICHO

Imebainika kwamba watoto 4 kati ya 25 waliofukuliwa kutoka kaburi la pamoja kwenye kaunti ya Kericho walifariki kutokana na majeraha ya kichwa, huku wengine 10 wakifariki baada ya kuzaliwa kabla ya siku zao kufika. Kulingana na ripoti ya upasuaji wa maiti iliyoongozwa na mwanapatholojia wa serikali Dakta Richard Njoroge, miili ya waathiriwa ilikuwa katika hatua […]

SERIKALI YAVUNJA KIMYA CHA PASIPOTI

Maswali yameendelea kuibuka kuhusu ni kwanini serikali imechukua muda mrefu kutoa msimamo wake kuhusu taarifa za kuwapa paspoti za usafiri makamanda wa kundi la wapiganaji la RSF nchini Sudan, na badala yake kujitokeza hapo jana baada ya wiki kadhaa kukanusha taarifa hizo. Katibu mkuu katika idara ya uhamiaji Dakta Belio Kipsang, amesema suala hilo linaangaziwa […]