DROO YA FA CUP 5TH ROUND

Droo ya raundi ya 5 ya dimba la FA Cup nchini Uingereza ilikamilika hapo jana, huku zawadi ya klabu ya Mansfield ya League One kuibandua Burnley ya ligi kuu, EPL, na kutinga awamu ya 5 ya FA baada ya miaka 50 ikiwa ni kukutanishwa na viongozi wa EPL Arsenal katika uwanja wa One Call. Manchester […]

TIMU 8 KUFAHAMU WAPINZANI KWENYE ROBO FAINALI CAF LEO

Klabu 8 zilizotinga awamu ya robo fainali ya klabu bingwa barani Afrika CAF Champions League zitafahamu wapinzani wao kwenye droo itakayofanyika hii leo jijini Cairo, Misri kufuatia kukamilika kwa awamu ya makundi Jumapili. Timu hizo zilikuwa kwenye makundi 4, ya kwanza na ya pili zikifuzu robo fainali. Miamba wa soka barani wamefuzu awamu hiyo, huku […]

SERIKALI YAANZISHA UJENZI WA THIKA STADIUM

Serikali imeanzisha ujenzi wa uwanja wa Thika Stadium wenye uwezo wa kuwabeba mashabiki 10,000, ambao huenda ukatumiwa kwa mazoezi wakati wa dimba la mataifa bingwa barani Afrika mwaka ujao, AFCON 2027. Ujenzi huo umekadiriwa kugharimu shilingi milioni 850, serikali ikisema utakamilika kufikia mwishoni mwa mwaka huu. Thika Stadium inatarajiwa kuchukua mahala pa Thika Municipal Stadium […]

SAFARI ZA NDEGE ZASAMBARATIKA

Shughuli za usafiri katika viwanja vya ndege nchini zinatarajiwa kuendelea kutatizika kutokana na mgomo wa wafanyakazi wa viwanja hivyo ambao wameapa kuendelea na mgomo wao licha ya agizo la mahakama kuwataka wasitishe mgomo huo. Hapo jana, wasafiri walilazimika kusalia ndani ya ndege huku wengine wakifutilia mbali safari zao kutokana na ukosefu wa wafanyakazi wa kudhibiti […]

FAMILIA, WANAHARAKATI WASHINIKIZA HAKI KITENGELA

Wanaharakati na familia ya Vincent Ayomo, mwanamme aliyeuawa Jumapili iliyopita katika eneo la Kitengela kwenye mkutano ulioongozwa na katibu mkuu wa ODM Edwin Sifuna, wameshinikiza uchunguzi wa kina kufanywa ili wapate haki. Ikiongozwa na mjane wake Winnie Ayomo, familia hiyo imesisitiza kuwa jamaa yao aliuawa na polisi waliiokuwa wakiutawanya umati, huku wanaharakati wakimtaka Waziri wa […]

UPINZANI KUONGOZA MAANDAMANO YA WATU 100,000 NAIROBI

Viongozi wa upinzani nchini wametangaza kuongoza maandamano makubwa jijini Nairobi Ijumaa wiki hii kushinikiza kuwajibishwa kwa maafisa wa polisi wanaoaminika kuvuruga ibada iliyokuwa ikihudhuriwa na aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua mwezi jana kaunti ya Nyeri, baada ya juhudi zao kukutana na Inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja kufeli hapo jana. Wakizungumza kwenye mkutano uliosambaratishwa na […]

MAHAKAMA KUTOA UAMUZI KWENYE KESI YA MVUVI NAKURU

Maafisa 6 wa idara ya wanyamapori nchini KWS wanaohusishwa na kutoweka kwa mvuvi Brian Odhiambo mwanzoni mwa mwaka jana katika mbuga ya wanyama ya Lake Nakuru watafahamu iwapo wana kesi ya kujibu au la tarehe 3 mwezi ujao. Kulingana na hakimu mkuu wa mahakama ya Nakuru Kipkurui Kibelion, mahakama itazingatia ushahidi uliotolewa na upande wa […]

SERIKALI INACHUNGUZA ‘MGENI’ ALIYEWAHADAA WANAWAKE

Hofu imeibuka kuhusiana na usalama wa wanawake nchini kutokana na ripoti ya raia mmoja wa kigeni kudaiwa kuwahadaa wanawake kadhaa na kuwapeleka katika makazi yake nchini, akarekodi na kusambaza picha za siri za wanawake hao bila idhini yao wala ufahamu wa idara ya ujasusi. Kulingana na msemaji wa serikali Isaac Mwaura, idara ya usalama, upelelezi […]

LEBRON HAJUI MUSTAKABALI WAKE NBA

Nyota wa mpira wa kikapu wa LeBron James amesema hana uhakika kama ataendelea kucheza zaidi ya msimu huu, ambao ni wa 23 kwake katika ligi ya mpira wa kikapu ya Marekani. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 41, anayekipiga katika klabu ya Los Angeles Lakers, alizungumza kabla ya mchezo wa nyota bora wa ligi hiyo, […]

AMBANI ALALAMIKIA UKOSEFU WA MABAO

Kocha wa AFC Leopards, Fred Ambani, amelalamikia ukosefu wa umakini wa kutikisa nyavu baada ya timu yake kutoka sare ya bila mabao dhidi ya Bandari katika Uwanja wa Mbaraki, jana. Licha ya sare hiyo, Ambani aliwasifu wachezaji wake kwa kuonyesha moyo wa kupambana chini ya hali ya hewa ya ukanda wa pwani aliyoitaja kuwa ngumu na […]